mtoto.news

Njaa Yawaangamiza Watoto wa Uganda

June 14, 2022

Zaidi ya watu nusu milioni wanakabiliwa na njaa huko Karamoja kaskazini mashariki mwa Uganda.

Katika mojawapo ya maeneo yaliyo na umaskini mno na yaliyosahaulika Nchini Uganda, Mama anampakata mwanawe aliyabakia mifupa tu, huku akiwa hanani, kwani anaogopa kwamba, mwanawe anaweza kuwa mwathiriwa mwengine tu atayetokomeshwa na njaa maeneo ya Karamoga.

Kulingana na France 24 Misiba ya asili, tauni ya nzige na viwavi jeshi, pia uvamizi unaofanywa na wezi wa mifugo wenye silaha, umewaacha wakazi wa Karamoga na chakula kidogo mno.

Wakaazi hawa wanatatizika kuweza kuishi, kwani maafa haya ya uhaba wa chakula hayakuanza leo wala jana.

“Katika kipindi cha miezi mitatu tumepoteza zaidi ya watoto 25 waliokuwa na umri wa chini ya miaka mitano kutokana na utapiamlo,” alisema Daktari Sharif Nalibe, afisa wa afya wa wilaya ya Kaabong, mojawapo ya wilaya zilizoathirika zaidi na Karamoja.

“Na hawa ndio waliokuwa chini ya uangalizi wetu, tena waliletwa katika dakika ya mwisho hospitalini. ila kuna wengi wanaofariki bila ya kuripotiwa katika jamii.”

Wakati tahadhari ya kimataifa inaegemea upande wa migogoro ya hali ya juu kama vile vita vya Ukraine na Ukame ulio katika Pembe ya Africa, Maafa ya Watoto wa Karamoja hayapewi kipaumbele.

Kutokana na tathmini ya mashirika ya kibinadamu na wafadhili wa kigeni, Zaidi ya watoto 91,000 na wanawake 9,000 wajawazito au wanaonyonyesha, wanasumbuliwa na utapiamlo mkali na wanahitaji matibabu ya haraka.

“Katika suala la utapiamlo uliokithiri, mwaka huu tumepitia hali mbaya zaidi ambayo tumekuwa nayo katika miaka 10 iliyopita,” alisema Alex Mokori, mtaalamu wa lishe kutoka UNICEF, ambayo inachunguza utapiamlo huko Karamoja na mamlaka za mitaa.

Kwa mara nyingi watoto wa Karamoja hulala njaa, au hula chakula kinachoweza kuwaathiri aina hii au nyingine.

Yajayo ni Mazito Zaidi

Kwa kuwa na mpaka na biashara haramu inayostawi, Karamoja imevumilia miongo kadhaa ya uvamizi wa ng’ombe wenye silaha kati ya koo za kuhamahama ambazo zinazunguka mpaka kati ya Uganda, Sudan Kusini na Kenya.

Aidha, Uvamizi huu unafanya maisha kuwa duni zaidi kwa jamii za Karimojong zinazotegemea mifugo na mazao ili kuishi, na uingiliaji kati wa serikali kuwapokonya wezi silaha haujakomesha mzunguko wa vurugu.

Karamoja inakabiliwa na ukame mkali, lakini mwaka jana ilishuhudiwa mafuriko na maporomoko ya ardhi hii ikizidisha ugumu wa maisha katika eneo hilo.

Nangole Lopwon alienda kuuza kuni katika kijiji cha jirani na kuwaacha mapacha wake wenye njaa na mmoja wa watoto wake wakubwa, na kurejea na kupata mmoja wa watoto hao amefariki.

“Ningefanya nini? Mtoto hakuwa mgonjwa. Ni njaa ndio iliyomuua,” mama wa watoto watano kutoka Kaabong alisema.

Sasa yeye pia hana lishe bora, na pacha aliyebaki yuko katika hali mbaya.

“Hata huyu anakaribia kufa,” alifoka.

Maafa ya Watoto wa Uganda hayapewi mtizamo wowote ule, kwani ulimwengu unazingatia vita vya Ukraine na Ukame ulio Katika Pembe ya Afrika.

Mwandishi-Khadija Mbesa

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *