mtoto.news

Hofu ya Kuongezeka kwa Unyanyasaji wa Ngono na Kijinsia wakati Uchaguzi Unakaribia

July 7, 2022

Kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2007/2008,Tume ya Uchunguzi kuhusu Ghasia za Baada ya Uchaguzi (CIPEV), ilirekodi kesi 900 za unyanyasaji wa kijinsia unaofanywa na maafisa wa usalama, vikundi vya wanamgambo na raia dhidi ya wanaume, wavulana, wanawake na wasichana katika muktadha wa unyanyasaji mkubwa, uhamishaji wa watu wengi na vifo zaidi ya 1,000.

Harakati za MULIKA WABAKAJI zimeshika kasi, kwani tunakaribia uchaguzi wa mwaka wa 2022, na hofu iko palepale kuhusu unyanyasaji wa ngono na unyanyasaji wa kijinsia kwa ujumla.

Mulika Wabakaji Campaign Consortium (MWCC), ni mkusanyiko wa zaidi ya Asasi za Kiraia 30.
Mashirika yanayoshughulikia Haki za Kibinadamu na Jinsia pamoja na amani, usalama na maendeleo yafanya ramani ya matukio na uchambuzi wa uwezekano wa unyanyasaji wa kijinsia kuongezeka wakati wa Uchaguzi wa mwaka wa 2022 nchini Kenya

Akizungumza leo hii, Mkurugenzi wa International Peace Brigade, Bwana Alberto Fait alisema kwamba, Waathiriwa wengi hawana imani au wamekumbana na unyanyapaa au kuhisi woga na hivyo kushindwa kuripoti kesi zozote zinazohusiana na sgbv, hii ikisababisha kiwango kikubwa cha unyanyasaji wa kijinsia.

Florence Mwikali, Mwanachama wa International Peace Brigade, aliongezea kusema kwamba, Waathiriwa hunyimwa huduma za kimsingi, haswa wakati ambapo hospitali za umma zitafungwa na hakutakuwa na upatikanaji wa matibabu n.k.

Akisisitiza kwamba, watoto pia wako katika mafuta moto wakati huu wa uchaguzi, kwani shule nyingi zitakapofungwa basi kutachochea ongezeko kubwa la kesi za watoto kunajisiwa.

Mulika Wabakaji wanatia juhudi zao zote katika kubadilisha simulizi la Unyanyasaji wa ngono na kijinsia.

Aidha, Mulika Wabakaji wanawania kufuatilia afya ya akili ya sio tu mwathirika, bali pia mhusika. kwani unyanyasaji huu wa kijinsia huweza kuwa mzunguko wa ubakaji na unajisi.

WITO KWA VYOMBO VYA HABARI

Mulika Wabakaji imewataka wanahabari wawe na umakinifu wakati wanatoa taarifa nyeti au hadithi kuhusu waathiriwa walioponea kutokana na unyanyasaji wa kingono na kijinsia.

Inaweza kuwa hadithi tu kwa mwandishi wa habari, lakini kiwewe kwa mwathiriwa.

MWITO KWA SERIKALI

Maggie Adhiambo, ameitaka serikali kushughulikia suala la msaada wa kisheria kwa wahasiriwa wa unyanyasaji wa kijinsia mahakamani, haswa katika kuwasaidia kupata haki.

Zaidi ya hayo, Adhiambo atoa wito kwa serikali kuongeza mgao wa bajeti kwa maeneo salama ikiwa ni pamoja na nyumba zenye usalama kwa waathiriwa wa SGBV.

Vile vile kuna haja ya kuwa na mahakama maalumu kwa ajili ya kesi za unyanyasaji wa kijinsia.

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *