mtoto.news

Msaada wa Vifaa Maalum kwa Watoto Wenye Ulemavu

July 7, 2022

Shirika la Plan International, pamoja na Kaunti ya Homa Bay wameshirikiana na Chama cha Walemavu wa Kimwili cha Kenya (APDK) na kutoa msaada wa vifaa kwa watoto Thelathini na sita wenye ulemavu.

Vifaa hivyo vyenye thamani ya KSh milioni 1.3 ni pamoja na viti maalum (viti vya magurudumu), vifaa vya kusimama, viatu vya mifupa na buti, AFOS, kiwiko cha mkono, fremu ya kutembea zilizo na magurudumu, miongoni mwa vitu vingine.

Akizungumza wakati wa zoezi la uchangiaji katika Chuo cha Sero Vocational, Afisa wa Miradi wa Shirika la Integrated Plan International, Joseph Mwita, alisema kwamba, shirika hilo lilishirikiana na APDK katika kutoa tathmini kwa watoto hao pamoja na vifaa saidizi vya kuwasaidia kupata haki zao za msingi ikiwemo elimu.

“Tumewapa vifaa kadhaa kama inavyopendekezwa na wataalamu ambavyo vingine ni kwa madhumuni ya kurekebisha na vingine vitatoa msaada katika suala la uhamaji, kwani tumegundua kuwa watoto hawa wameachwa nyuma na mara kwa mara hawasaidiwi ipasavyo ili kuwawezesha kufurahia haki zao za msingi kama vile elimu na huduma za matibabu.” alisema.

Mwita alisema kwamba Plan International inajenga uelewa unaolenga jamii pamoja na wazazi katika nia ya kubadilisha mtazamo wao kuhusu watoto wenye ulemavu.

“Afua hizi zinalenga kubadili mtazamo wa wazazi ili kuhakikisha kwamba, wanawaleta watoto kwa ajili ya tathmini,” alisema Mwita.

Mwita alisema kuwa, mpango huo unafanywa katika maeneo matatu ya Mbita, Rangwe na Asego ndani ya Kaunti ya Homa Bay.

Alitoa wito kwa washikadau wote ndani ya kaunti ikiwemo serikali ya kaunti na ile ya kitaifa kufanya kazi pamoja na kuwasaidia watoto hao.

Dk Kenneth Ambuchaba, anayefanya kazi katika Hospitali ya Taaluma na Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga, alisema kuwa, watoto hao wanakabiliwa na ugonjwa wa kuzaliwa nao unaojulikana kwa jina la Utindio wa Ubongo ‘cerebral palsy,‘ kama inavyoonyeshwa kwenye tathmini zao, huku akiongeza kuwa, ugonjwa huo unasababishwa na mabadiliko ya jeni, maambukizi ya fetusi na ukosefu wa usambazaji wa oksijeni kwa ubongo wa fetasi.

Utindio wa Ubongo ‘cerebral palsy‘ husababisha matatizo katika kutembea, usawa wa misuli , makao n.k kwa watoto.

Alikariri kuwa, vifaa vilivyotolewa haviwezi kuondoa ugonjwa huo kikamilifu, “Vifaa hivi haviwezi kurekebisha ulemavu kikamilifu. Tunachofanya ni kuzuia watoto kupata ulemavu wa kudumu,” alisema Odhiambo.

Aliwataka wazazi kuwapeleka watoto wao kwa matibabu, na kuongeza kuwa, kuna changamoto zinazotokana na kupooza kwa ubongo ilhali hawajui jinsi ya kuzishughulikia.

“Hii ni changamoto kwa wazazi kwa sababu hawajui jinsi ya kukabiliana na watoto hawa kwani wengi wao hawawezi kuzungumza, kutembea au kukaa kwa kujitegemea na hivyo wanahitaji msaada,” alisema.

Wazazi hao walishukuru shirika hilo kwa msaada huo wakisema kuwa, vifaa hivyo ni vya bei ghali na kwamba hawakuweza kumudu kununua wenyewe.

Nancy Akoth, mama wa mtoto aliye na Utindio wa Ubongo ‘cerebral palsy‘ alisema kwamba, haikuwa rahisi kuhama kutoka mahali pamoja hadi pengine na mtoto wake wa miaka miwili ambaye hawezi kusimama wala kukaa bila msaada.

Alieleza kwamba, alikuja kujua hali ya mwanawe alipokuwa na umri wa miezi mitano na hakuweza kuketi peke yake bila msaada.

“Nilipompeleka hospitalini ndipo nilipojua kwamba alikuwa na Utindio wa Ubongo ‘cerebral palsy‘ na leo tumepokea vifaa hivi ambavyo ni muhimu sana kwetu,” alisifu.

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *