mtoto.news

Kwa nini Sheria ya Afya ya Ujinsia na Uzazi inapingwa Afrika Mashariki?

July 22, 2022

Nchi sita za Jumuiya ya Afrika Mashariki – Burundi, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Uganda na Tanzania – hivi karibuni zimehitimisha mikutano ya hadhara kuhusu mswada mpya wa afya ya uzazi na ujinsia. 

Wafuasi wa Mswada huo wanasema kuwa, sheria hii itaboresha upatikanaji wa afya ya ngono na uzazi ambayo, kwa upande wake, itaboresha viashirio vingine vya afya ya umma na maendeleo kama vile vifo vya uzazi na viwango vya maambukizi ya VVU.

Mswada huo, unaolenga kuboresha upatikanaji wa huduma za afya ya ujinsia na uzazi kwa wanawake na wasichana katika nchi sita za Afrika Mashariki unakabiliwa na vita vikali vya kuidhinishwa, huku upinzani kutoka kwa wahafidhina wanaodai kuwa utakuza uavyaji mimba na haki za LBGTQ.

Kupingwa kwa mswada huo pia kumetokana na ikhtilafu kwamba, utoaji wa elimu ya kina ya kujamiiana kwa vijana, itawasukuma watoto kujihusisha kwenye ngono za mapema.

Huku wengine wanahoji, ni kwa nini serikali iwajibike kutoa elimu ya ngono kwa watoto badala ya wazazi?

 Kifungu cha utoaji mimba kinakabiliwa na upinzani mkubwa zaidi, kwani wapinzani wanapinga ufafanuzi wa uavyaji mimba katika Mswada huo na wanahoji kuwa hauakisi maadili ya Kiafrika katu, huku Wanadai kwamba, ikiwa sheria hiyo itapitishwa, basi Mswada huo unafaa kufanya huduma za uavyaji mimba kupatikana iwapo tu itahitajika.

karibu theluthi moja ya wanawake wote walio katika nchi zinazoendelea wanajifungua wangali watoto, na ni wazi kuwa dunia haiwapatii kipaumbele watoto hawa,
Kulingana na mimba tunazoziona za mara kwa mara miongoni mwa akina mama walio bado wadogo ni ishara tosha kwamba wanahitaji sana taarifa na huduma za afya ya uzazi na kujamiiana.”

MKURUGENZI MTENDAJI WA UNFPA DK NATALIA KANEM

Kulingana na UNFDA, Matatizo katika ujauzito na uzazi ndiyo chanzo kikuu cha vifo miongoni mwa wasichana wenye umri wa miaka 15 hadi 19, ambao pia wana uwezekano mkubwa wa kukumbwa na orodha ya ukiukwaji mwingine wa haki zao za binadamu, hii ni kuanzia ndoa za kulazimishwa na ukatili wa karibu hadi madhara makubwa ya afya ya akili kwani watoto hawa hujifungua wakati wao bado hawajatoka utotoni mwao.

Mwishowe, wakosoaji wanapinga sehemu ya ‘surrogacy”, wakidai maadili haya hupotoka kwenye utaratibu wa uumbaji na inaruhusu watu binafsi wa LGBT kupata watoto.

Viongozi wachache wa Kiislamu nchini Kenya na Tanzania wanakataa upigwaji marufuku wa ndoa za utotoni na wanahoji kuwa mara tu hedhi inapoanza, msichana anaweza kuolewa bila ya kujali umri wake.

Je wewe maoni yako ni gani?

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *