mtoto.news

Ripoti 2021: Ukiukaji Uliovuka Mipaka

July 22, 2022

Kulingana na Ripoti ya 2021 kuhusu Watoto na Migogoro ya Kivita , angalau wasichana 5,242 na wavulana 13,663 wamekuwa wahasiriwa wa ukiukaji mkubwa, huku watoto 1600 wakiwa wahasiriwa wa ukiukaji wa mara kwa mara.

Ripoti hiyo iliangazia jumla ya ukiukaji wa kuvuka mipaka wa watoto 23,982.

Ujumla wa nambari hii ya ukiukaji iko sawa na idadi ya mnamo mwaka wa 2020, inayoonyesha wastani wa ukiukaji 65 kwa siku.

wahalifu wa ukiukaji asilimia 15 hawakuweza kutambuliwa,hii ikifanya uwajibikaji kuwa mgumu zaidi.

wasichana walizidi kuathiriwa na ukiukaji mkubwa, unaojumuisha hadi asilimia 30 ya waathiriwa wote, hii ilichochewa na Mashambulizi dhidi ya shule na hospitali.

Ripoti hii, ina maelezo zaidi kuhusu uelewa zaidi wa mwelekeo wa kijinsia katika ukiakaji wa haki za watoto wakati wa migogoro

Mwaka wa 2021 umeshuhudia mseto muovu wa kuongezeka kwa migogoro, mapinduzi, unyakuzi na ukiukwaji wa sheria za kimataifa.

Hakuna neno lililo na mizani ya kutosha linaloweza kuelezea hali ambayo watoto walio kwenye vita na migogoro wamestahimili.

Wale walioweza kuponea chupuchupu wako katika hatari ya kuathirika maisha yao yote kutokana na makovu mazito ya kihemko na kimwili.

Licha ya takwimu za kutisha za mwaka wa 2021 zilizomo katika ripoti hiyo, pia kulikuwa na maendeleo makubwa yaliyopatikana katika baadhi ya miktadha. Kwa ujumla, watoto 12,214 waliachiliwa kutoka kwa vikosi vya kijeshi na vikundi katika nchi zilizo kwenye ajenda ya CAAC, hii ikijumuisha Jamhuri ya Afrika ya Kati, Colombia, DRC, Myanmar, na Syria.

watoto walioachiliwa kutoka kwa vikosi vya kijeshi na vikundi wanapaswa kufaidika na usaidizi endelevu, wa jumla, wa jinsia na umri na pia kusaidiwa katika kujumuishwa kwenye jamii.

Ripoti hii inatoa wito kwa kila mtu kuhakikisha usalama wa watoto wakati wa migogoro, huku ikiwataka kumaliza ukiukaji mkuu wa watoto.

Ripoti hii imetaka pande zote zinazohusika katika mizozo, iwe ni vikosi vya serikali au vikundi visivyo vya serikali, kuruhusu ufikiaji wa wataalam wa ulinzi wa watoto na watendaji wa kibinadamu kufanya kazi yao ya kuokoa maisha na kuweka kipaumbele kwa ufikiaji wa kibinadamu kwa watoto walio katika migogoro na vita vya silaha.

Wakati amani itadudumia, basi watoto ndio watakuwa wakwanza kuathirika.

Amani lazima itawale kwani ndiyo njia pekee endelevu ya kukomesha na kuzuia ukiukwaji mkubwa dhidi ya watoto katika migogoro ya kivita. Katika ulimwengu ambao bado umeathiriwa na janga la COVID-19 na ambao umekumbwa na uhaba wa rasilimali na majanga ya muda mrefu na mapya, ni muhimu zaidi kuchukua hatua ili kuwalinda watoto na kuhakikisha maisha yao ya baadaye yako salama

MWAKILISHI MAALUM WA KATIBU MKUU WA WATOTO NA MIGOGORO YA KIVITA, VIRGINIA GAMBA.

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *