mtoto.news

Msichana,15, Awaua Ndugu Zake 3 na Binamu

August 29, 2022

Maafisa wa upelelezi katika Kaunti ya Kiambu wanachunguza kisa ambapo mwanafunzi wa kidato cha kwanza anadaiwa kuwaua ndugu zake watatu na binamu yake katika muda wa mwaka mmoja uliopita.

Kulingana na KBC, Mtoto huyo alipokuwa katika kituo cha Polisi cha Kikuyu, alikiri kwa wapelelezi jinsi alivyowaua ndugu zake, mmoja akiwa na umri wa miezi 15, mwengine miaka 5 na mwengine akiwa na miaka 7, mauaji yaliyotokea kati ya Februari na Julai 2021.

Vile vile, mtoto huyo alikiri kumuua binamu yake aliyekuwa na umri wa mwaka mmoja na miezi sita, hapo kijijini Gathiga, kaunti ndogo ya Kabete, Alimuua mtoto huyo kwa kumzamisha kwenye kisima katika boma lao mwezi Julai wakati wa mapumziko ya shule.

Mapema Jumapili, babake msichana huyo alitembea hadi kituo cha polisi cha Kikuyu na kujaza ripoti dhidi ya msichana huyo wa miaka 15 ambaye alimtuhumu kuwaua watoto wake watatu.

Mtoto huyo alikiri kutekeleza mauaji hayo mbele ya afisa wa watoto katika kaunti ndogo ya Kikuyu.

Kwa sasa yuko kizuizini katika kituo cha Polisi cha Kikuyu huku wapelelezi wakimshughulikia ili afikishwe mahakamani.

Afisa wa Uchunguzi wa Jinai katika Kaunti Ndogo ya Kikuyu George Muriuki alisema kwamba uchunguzi utakapokamilika mshukiwa atakabiliwa na sheria.

 

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *