mtoto.news

Kenya Yashika Mkondo wa Uafikishaji wa Lengo la Upatikanaji wa Elimu kwa Wote

August 30, 2022

 

Mtaalamu Mwandamizi wa Mpango wa Elimu katika Ofisi ya Kanda ya Afrika Mashariki ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO),Saidou Sireh Jallow, aliliambia kongamano la elimu kuwa Kenya imeweka kipaumbele katika uwekezaji wa umma katika elimu, hii ikisababisha mwelekeo wa kupanda kwa viashiria vingi vya maendeleo ya elimu. .

“Kenya pia imetekeleza mpango wa kujifunza kidijitali ambao umeongeza ufikiaji wa elimu,” Jallow alisema wakati wa kongamano la kitaifa la mashauriano kuhusu kubadilisha elimu nchini Kenya.

Aliendelea kusema kwamba, taifa hili la Afrika mashariki limetekeleza mageuzi muhimu katika sekta ya elimu ambayo yameboresha matokeo kwa wanafunzi.

Afisa huyo wa UNESCO alifichua kuwa, Kenya pia imeunda na kutekeleza sera zinazoimarisha ushirikishwaji katika elimu ikiwa ni pamoja na sera ya kujiunga tena ambayo imeongeza kasi ya nchi katika kuelekea kwa mabadiliko ya asilimia 100 kutoka elimu ya msingi hadi ya upili.

Jallow aliongezea kusema kuwa, Kenya pia imewekeza elimu ya wasichana ili kufikia usawa wa kijinsia katika sekta ya elimu.

Kenya imeimarisha usimamizi wa data ya elimu kwa ajili ya kupanga na kuripoti katika viwango vyote.

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *