mtoto.news

Wazazi waghadhabishwa na picha za watoto wakitoa kuku manyoya wakati wa mafunzo ya CBC

September 19, 2022

Wazazi wengi wameonyesha hasira yao mitandaoni baada ya picha ya wanafunzi wakitoa kuku manyoya kusambaa mitandaoni.

Wananchi walionyesha wasiwasi kupitia twitter, huku wakikashifu mtaala wa CBC na wakisema kwamba, usalama wa watoto hao haukuzingatiwa kamwe, kwani kulikuwa na utumiaji wa visu na maji ya moto wakati wa matayarisho hayo ya kuku.

Wengine wanadai kwamba, huu ni uwizi hadharani kwani shule zingine zinaitisha senti kutoka kwa watoto kwa madai ya minajili ya mafunzo ya uanzisho wa pesa kihistoria.

Mwalimu Dida pia ameeleza kusikitishwa kwake na mfumo wa CBC akidai kwamba, haujafikia matarajio aliyokuwa nayo hapo awali.

 

Kila jambo lililo na ubaya, pia lina uzuri wake, hata baada ya wanamitandao wengi kukashifu mfumo wa CBC bado kuna wengi ambao wanauunga mkono.

Wizara ya Elimu imekimbilia kutetea Mtaala Unaozingatia Umahiri (CBC)baada ya kuwepo na hofu ya uwezekano wa mtaala huo kufanyiwa marekebisho au kufutiliwa mbali kabisa na serikali mpya.

Kupitia taarifa ya kwanza ya utekelezaji ya CBC-Volume 1, Katibu wa Baraza la Mawaziri la Elimu Prof George Magoha anasema kuwa mfumo wa elimu wa 8-4-4 ulioanzishwa zaidi ya miaka 30 iliyopita ulikuwa umepita manufaa yake.

“Mazingira ya sasa ni tofauti sana na mfumo wa elimu wa 8-4-4. Sasa tuko katika jamii inayotegemea maarifa inayokabiliwa na changamoto, vikwazo na fursa zinazobadilika kila mara. Hii inahitaji aina mpya ya elimu…elimu ambayo inawapa wanafunzi sio ujuzi tu, bali pia uwezo wa kujifunza, ” Magoha anasema.

Hata hivyo, Mwanamtandao alitoa maoni na kusema kwamba, wanafunzi ndio wanafaa kupewa kipaumbele kwani mfumo huu umewekwa kwa ajili ya manufaa na mwanafunzi na wala sio kwa lingine lile.

Aidha, shule nyingi za kibinafsi zimetoa maridhio yao ya kuchagua Mtaala wa Kimataifa iwapo CBC itafutiliwa mbali.

 

 

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *