Familia moja mjini Mombasa inaomboleza kifo cha watoto wawili wanaodaiwa kunyongwa hadi kufa na baba yao na kuchomwa ndani ya nyumba yao eneo la Bombolulu Workshop.
Jason Chacha, mzee wa miaka 55 na baba wa watoto watatu wanasemekana kuwaua watoto hao wawili wenye umri wa miaka 4 na 8 mtawalia Jumatatu saa 2 asubuhi alafu kutoroka.
Kulingana na mkewe Maria Boke, kisa hicho kilitokea baada ya mumewe wa ndoa ya zaidi ya miaka 10 kumtishia kuondoka nyumbani la sivyo angemuua Jumapili usiku.
“Nimepitia changamoto nyingi sana kwenye ndoa yangu kwa muda mrefu lakini sijawahi kufunguka kwa mtu yeyote. Nimekumbana na ukatili wa kupita mipaka kutoka kwa mume wangu ikiwemo kunipiga lakini mambo yalizidi kuwa mabaya wiki hii,” alisema.
Leave a Reply