mtoto.news

Kenya: Wadau wa Elimu Wajitolea Kufundisha usimbaji(coding)Shuleni

October 7, 2022

KAIS, Kodris wafanya kongamano la kuhamasisha washikadau kuhusu umuhimu wa kufundisha usimbaji kwa wanafunzi wachanga.

Chama cha Shule za Kimataifa cha Kenya (KAIS) kwa ushirikiano na kampuni ya Education Technologies, Kodris Africa na Kenya Commercial Bank waliitisha kongamano la ujuzi wa Kidijitali mnamo Alhamisi lililowaleta pamoja wadau mbalimbali kutoka sekta ya elimu na ICT.

Tukio hilo lilijikita katika mtaala wa kompyuta na usimbaji (coding)na umuhimu wa kujumuisha ujuzi wa kidijitali katika shule za msingi na upili.

Pia yalikuwepo makampuni makubwa ya teknolojia kama vile Microsoft, Google, Safaricom na Liquid Telcom miongoni mwa mengine.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Jane Mwangi, Mkuu wa Sekretarieti ya KAIS, alisisitiza haja ya kuwafunza wanafunzi kuhusu ujuzi wa kidijitali kuanzia ngazi ya msingi akisema, “Ukiangalia nchi zilizoendelea zaidi kama Singapore na Japan, zimekuwa zikiwafundisha wanafunzi wao kuandika msimbo kutoka ngazi ya awali,” alisema.

Jack Ngare, mkuu wa Google barani Afrika alisema kwamba, njia pekee ya Kenya na Afrika kusalia sawa na mataifa yaliyoendelea ni kwa kuanzisha usimbaji katika ngazi ya shule ya msingi. 

Mkurugenzi Mtendaji, Kituo cha Maendeleo cha Microsoft Africa, Catherine Muraga aliongeza kuwa kuandika misimbo(coding) imekuwa muhimu sana kwa njia zote za kazi na kuongeza kunena, “haja ya kufundisha wanafunzi jinsi ya kutatua matatizo kupitia usimbaji imekuwa muhimu zaidi na inahitaji kuzingatiwa.

Usimbaji ni muhimu kama Kiingereza au Kifaransa katika mawasiliano na hivyo inabidi tuhakikishe kwamba watoto wetu wanakuwa na vifaa vya kutosha kwa ajili ya ufanisi na tija.”

Kodris Africa ndilo shirika pekee linalotoa mtaala ulioidhinishwa na Taasisi ya Ukuzaji Mitaala ya Kenya (KICD). 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kodris Africa, Mugumo Munene alisisitiza umuhimu wa kufundisha wanafunzi zaidi ya jinsi ya kutumia programu za kompyuta. 

Ulimwenguni, ajira katika kazi za kompyuta na IT inakadiriwa kukua asilia 13 kutoka mwaka wa 2020 hadi 2030, asilimia ya juu kuliko wastani wa kazi zote.

Mshahara wa wastani wa kila mwaka wa kazi za IT ulikuwa dola 91,250 mnamo Mei 2020, ambayo ilikuwa juu kuliko mshahara wa wastani wa kila mwaka wa kazi zote ambazo zilikuwa zinasalia dola $41,950 kwa mwaka.

Mahitaji ya ujuzi wa IT yanatarajiwa kuendeshwa na kompyuta ya wingu, mkusanyiko mkubwa wa data, uhifadhi, na usalama wa data.

Inakadiriwa kuwa kufikia mwaka wa 2030, asilimia 50 – 55 ya kazi zote nchini Kenya zitahitaji kiwango fulani cha ujuzi wa kidijitali huku mahitaji yakiendeshwa na makampuni yanayotumia teknolojia za kidijitali.

Katika miongo miwili iliyopita, marekebisho ya mitaala yamechochewa na mabadiliko ya haraka ya kiteknolojia na kijamii. 

Hata hivyo, ingawa umuhimu wa ujuzi wa kidijitali umetambuliwa, kumekuwa na mwelekeo mdogo hasa katika masoko yanayoibukia juu ya kiwango cha mahitaji ya ujuzi huu, na miundo inayoweza kutumika kuwafundisha.

Nchi kama vile Marekani, Uchina, Uingereza, Ujerumani na Ufaransa tayari ni miongoni mwa nchi nyingine nyingi katika ulimwengu zilizolazimisha kuwekwa kwa msimbo kwa wanafunzi wa darasa la kwanza.

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *