Mnamo 2022, tunaadhimisha kumbukumbu ya miaka kumi tangu kuzaliwa kwa Siku ya Kimataifa ya Msichana (IDG).
Katika miaka hii 10 iliyopita, kumekuwa na umakini mkubwa katika masuala ambayo ni muhimu kwa wasichana, haswa miongoni mwa serikali, watunga sera na umma kwa ujumla, pia kumekuwa na umuhimu chanya katika kuwapa wasichana fursa zaidi kwa kusikilizwa sauti zao katika jukwaa la kimataifa.
Hata hivyo, uwekezaji katika haki za wasichana bado ni mdogo na wasichana wanaendelea kukabiliana na changamoto nyingi ili kutimiza uwezo wao.
Wanawake na wasichana wananyimwa haki za kisheria sawa na wanaume na wavulana katika nchi nyingi za Afrika, ikiwa ni pamoja na linapokuja suala la ndoa.
Hii huweka mamilioni katika hatari kubwa ya ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwemo ndoa za utotoni, ubakaji kwenye ndoa, mimba za kulazimishwa, na unyanyasaji wa nyumbani.
Aidha, migogoro ya mara kwa mara na mabadiliko ya hali ya hewa na COVID-19 pia imechangia pa kubwa katika upuuzaji wa haki za wasichana.
Ni ukweli kwamba, wasichana kote ulimwenguni wanaendelea kukabiliwa na changamoto ambazo hazijawahi kushuhudiwa katu,hasa katika elimu yao, ustawi wao wa kimwili na kiakili, na ulinzi unaohitajika kwa maisha yasiyo na vurugu.
Hata hivyo, Uganda imeungana na mataifa mengine duniani katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya mtoto wa kike, huku serikali inayoshughulikia masuala ya watoto Afrika, ikizindua kampeni dhidi ya ndoa za utotoni na unyanyasaji wa watoto.
Wasichana wenye ulemavu wanakabiliwa na vikwazo vya ziada vya kupata usaidizi na huduma.
COVID-19 imezidisha mizigo iliyopo kwa wasichana kote ulimwenguni na kuondoa mafanikio muhimu yaliyopatikana katika muongo uliopita.
Pamoja na dhiki, hata hivyo, huja ujanja, ubunifu, ukakamavu, na ustahimilivu.
Wasichana milioni 600 duniani waliobalehe wameonyesha mara kwa mara kwamba kutokana na ujuzi na fursa, wanaweza kuwa wabadilishaji wa maendeleo katika jamii zao, na kurejesha nguvu kwa wote, wakiwemo wanawake na wanaume.
“Wasichana wanaposaidiwa kutambua haki zao za kibinadamu, basi wanaweza kufikia uwezo wa juu na kukusudia kuunda ulimwengu bora kwa wenyewe,” Katibu Mkuu António Guterres alisema katika ujumbe wake.
Wakati umewadia wa sisi sote kuwajibika katika kuwekeza haki na kutia maanani siku zijazo za watoto wa kike, huku tukiweka kipaumbele uongozi na uwezo wao.
Leave a Reply