mtoto.news

Makali ya Njaa yawaweka watoto nje ya madarasa

October 17, 2022

shule nyingi maeneo ya Turkana zimefungwa kutokana na Ukame, huku maelfu ya watoto wanaathiriwa na Utapiamlo

Shuleni Kavunzoni, watoto wengi wanalilia njaa huku wengi wao wakikosa kuwa makini darasani, ni misimu minne sasa isiyo na mvua mjini Ganze kaunti ya kilifi. Udongo umemumunyuka na ardhi imekomaa, watoto hawapati chajio wala kiamsha kinywa.

Imekadiria miaka mitano sasa, ambapo wenyeji hawajaweza kupanda wala kuvuna chochote kile,ila hio ndio hali ambayo watoto kama Moses wanaendelea kuvumilia kila kukicha.

Moses, Mwanafunzi kutoka shule ya msingi ya kavunzoni hana budi ila kujikakamua kwenda shuleni bila kupata mlo siku kadhaa.

wakati watoto hao wanasoma kuhusu vyakula mbali mbali darasani, Fikra za watoto wengi zinaenda kwingineko, kwani wengi wao hawajaona chakula kwa muda mrefu.

Moses Jackson anashindwa kuvumilia huku chozi lambubujika, na mwalimu akimuuliza kunani basi analia njaa ya siku kadhaa. Moses ni mmoja kati ya watoto milioni nne wanaohitaji msaada wa chakula kutokana na ukame nchini Kenya.

Chrispus Masha, Naibu mwalimu mkuu katika shule ya msingi ya kavunzoni, anaarifu kwamba watoto wengi wanakosa kwenda shuleni kwa sababu ya ukosefu wa lishe na maji ya kunywa. “Mtoto anaweza kukaa siku mbili au tatu bila chakula,” alisema bwana Masha.

Dennis Mramba, Meneja wa miradi World Vision, amesema kwamba wamefanya utafiti na kuweza kugundua kwamba, asilimia 24 ya watoto kutoka kijiji cha kavunzoni wana utapiamlo, na isitoshe asilimia 35 kati ya watoto ambao wako chini ya miaka mitano wako kwa hatari zaidi ya kupata utapiamlo.

UNICEF imeshirikiana na World Vision, serikali kuu na ya kaunti ya kilifi na World food program, na wameweka mikakati ya kuwanusuru wale walioathirika zaidi. Kaunti 29 nchini Kenya zaendelea kuvamiwa na baa la njaa, huku ukame unakita mizizi katika kaunti hizi. Watoto wengi wamelazimika kuacha shule ili kuweza kuwasaidia wazazi wao kutafuta maji na chakula.

Vile vile, shule nyingi maeneo ya Turkana zimefungwa kutokana na Ukame, huku maelfu ya watoto wanaathiriwa na Utapiamlo.

Akihutubia Bunge la Kaunti, Gavana wa Mandera, Mohamed Adan Khalif alisema, “Ukame pia umeathiri sekta yetu ya elimu kwani shule nyingi zinakabiliwa na dhiki ya kifedha na haziwezi kutoa chakula kwa wanafunzi wao. 

Tatizo la njaa linaweza kusababisha utapiamlo, kwa muda mrefu, huku ikichochea athari ya kudumu kwenye sekta ya elimu, kwa hivyo kuna haja ya kuchukua hatua za haraka, ikijumuisha usambazaji wa maji shuleni na kufikiria juu ya usambazaji wa chakula kwa shule 31 za bweni, na zaidi ya vituo 300 vya E.C.D katika Kaunti hiyo.

                                                                     Maudhui:Runinga ya Citizen

 

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *