mtoto.news

Wakenya 31 waokolewa kutoka kwa wateka nyara huko Laos

October 19, 2022

Utekaji nyara wa kuvuka mipaka bado unaendelea nchini Kenya.

Mnamo tarehe 31 Agosti 2022, HAART{Ufahamu Dhidi ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu}ilipokea ombi la kutaka usaidizi kupitia mitandao ya kijamii na barua pepe. Bwana mmoja aliwafahamisha HAART kwamba mwanafamilia wake ameshawishiwa kwa ahadi za uwongo za kufanya kazi Thailand ila alisafirishwa hadi Laos, pamoja na Wakenya wengine.

Kwa hofu, Bwana huyo aliiomba HAART kuingilia kati ili kuokoa kundi la Wakenya na kuwarejeshwa kwao. Shirika hilo liliweza kutafuta msaada kutoka kwa mashirika mbalimbali ya serikali, zikiwemo balozi katika nchi husika.

Aidha, mnamo tarehe 12 Septemba 2022, HAART ilipokea simu ya ahueni kutoka kwa mabalozi wa Kenya nchini Thailand wakiwafahamisha kuwa wamewaokoa Waathiriwa 31 nchini Laos na Myanmar.

Kundi la walionusurika lilifika salama nchini Kenya mnamo september na waathirika wote wanasaidiwa na wahudumu wa shirika la HAART  kupitia ushauri nasaha, uchunguzi wa kimatibabu, mahitaji ya msingi pamoja na uwezeshaji wa kielimu na kiuchumi ili kupunguza hatari ya kusafirishwa tena. Utaratibu ambao unaweza kuchukuwa hadi miaka miwili. Kufikia sasa, waathiriwa 24 wamepokea uchunguzi wa matibabu.

Waathiriwa hao wameshirikishwa katika uhalifu wa ngono mitandaoni huku wakitishwa kufichuliwa taarifa zao nyeti iwapo watakosa kutuma pesa.

Inakadiriwa kuwa idadi ya watoto wanaosafirishwa duniani kote ni milioni 5.5. Wanateseka kutokana na ukatili, unyonyaji na unyanyasaji, kazi ya kulazimishwa, ndoa za kulazimishwa, ukahaba, ombaomba na kuandikishwa kwenye vikundi vya kigaidi.

Vile vile watoto wengi nchini Kenya wako katika hatari ya kutekwa nyara haswa katika miji mikuu kama vile Nairobi, Kisumu na Mombasa.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu 2022: Serikali ya Kenya iliripoti kwamba, wameweza kuwatambua wahasiriwa 482 wa biashara hiyo ambao walikuwa wanawake 45, wavulana 111 na wasichana 326 ,ukilinganisha na mwaka 2021, kumekuwa na ongezeko kubwa ambapo serikali ilibaini wahanga 383 wa biashara hiyo.

Hata hivyo Kenya inafanya juhudi za juu ili kuweza kukabiliana na usafirishaji haramu.

 

Haart

 

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *