mtoto.news

Kaskazini mwa Kenya: Zaidi ya watoto laki sita wanakabiliwa na utapiamlo mkali

November 28, 2022

Ingawa ukame si jambo geni katika eneo hili, ukubwa na muda wa ukosaji mvua katika kipindi hiki haujawahi kushuhudiwa, na hali hii inazidi kuzorota kwa kasi katika maeneo kame na Nusu Kame nchini Kenya (ASAL). 

Kulingana na baraza la DRC (Danish Refugee Council), watu Milioni 2.1 kwa sasa wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula katika maeneo ya wafugaji kaskazini mwa Kenya.


Viwango vya utapiamlo vinaongezeka kwa kasi, huku ikijumuisha takriban watoto 652,960 wenye umri wa miezi 6-59 na wanawake 96,480 wajawazito na wanaonyonyesha  wanaohitaji matibabu ya utapiamlo uliokithiri (data ya IPC) ambao umesababisha matokeo mabaya ya muda mrefu katika ukuaji wa watoto hao. 

Upotevu wa malisho na vituo vya maji kwa mifugo umesababisha vifo vya zaidi ya ng’ombe milioni 1.5 maeneo ya ASAL. Mnamo Septemba pekee, zaidi ya mifugo 17,000 walikufa katika kaunti ya Mandera, wakiwemo ng’ombe, ngamia, kondoo na mbuzi. Mifugo ni rasilimali muhimu ya maisha na lishe kwa jamii nyingi za wafugaji, na kimsingi, maziwa safi ni chanzo kikuu cha lishe kwa watoto walio chini ya miaka mitano.

Ili kuelewa kikamilifu ukubwa wa mgogoro huo, DRC ilifanya tathmini ya mahitaji ya haraka katika kaunti za Turkana, Garissa, na Mandera, ikijumuisha mahojiano 258 ya watu binafsi kati ya tarehe 12-18 Septemba 2022. Kutokana na tathmini hiyo, DRC ilihitimisha kuwa asilimia 94 ya waliohojiwa waliripoti kuwa hawataweza kukidhi mahitaji ya kimsingi ifikapo mwezi october, wakati asilimia 18 waliripoti kwamba kulikuwa na watoto waliotengwa au wasio na wazazi katika jamii.

Kumekuwa na ongezeko la viwango vya unyanyasaji wa kijinsia na ukosefu wa usalama kwa ujumla na asilimia 82 ya wanawake walisema kuwa wanahisi kutokuwa salama katika jamii zao.

 

Hata hivyo kuna haja ya kupata vituo vya maji vilivyo salama, na kujizatiti katika kupunguza hatari zinazohusiana na ukusanyaji wa maji ikiwa ni pamoja na wasiwasi  kwamba watoto huweza kuanguka na kuzama kwenye visima vilivyo wazi .

 

Pia kuna haja ya kujumuisha Umri, Jinsia na Anuwai ili kuhakikisha upatikanaji wa msaada na ulinzi kwa UAMs, wazee, kaya zinazoongozwa na wanawake, watu wenye ulemavu, watu wenye magonjwa sugu, na watu wanaoishi katika maeneo ya mbali na wasio na uwezo wa kupata soko au vituo vya biashara.

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *