mtoto.news

Wito wa Ruto wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Hali ya Hewa

February 21, 2023

Mheshimiwa Rais William Ruto

Rais wa Kenya, William Ruto, aita wito wa Nchi zote Afrika, katika kuungana mkono ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Mataifa maskini, hasa yaliyomo barani Afrika, yameathiriwa vibaya na mabadiliko ya hali ya hewa, huku ikizidisha ukame na mafuriko.


Rais William Ruto amesema kwamba, sasa ni wakati muafaka kwa Afrika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa pamoja. Alisema kuwa, hatua madhubuti zitaonekana tu wakati juhudi za mataifa binafsi zitakapogeuzwa kuwa juhudi za pamoja.

Rais Ruto amenena kwamba bara la Afrika lazima lizungumze kwa sauti moja na kutetea matamanio ya watu wake.

Ni lazima tuwatetee watu wetu dhidi ya dhuluma inayochochea uporaji wa maliasili za Afrika” Alibaini.

Alikuwa akizungumza mnamo Ijumaa, hapo mjini Addis Ababa, Ethiopia, wakati wa kongamano la pili la Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kamisheni ya Mabadiliko ya Tabianchi ya Kanda ya Sahel. Mkuu huyo wa Nchi alibainisha kuwa, kwa Afrika, kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, ni suala la usalama wa binadamu.

Ruto alitoa wito wa kuwepo kwa “mfumo wenye haki zaidi wa kifedha” ambao utaleta pamoja hatua za hali ya hewa na fedha za maendeleo kwa Afrika. Alisema kwamba, mfumo wa aina hiyo utazalisha ajira kwa uendelevu, na pia utasababisha ahueni endelevu baada ya maafa na kuboresha ushirikishaji hatarishi.

Mabadiliko ya hali ya hewa ni tishio kubwa linalowakabili watoto wote duniani. Mabadiliko ya hali ya hewa huleta tishio kubwa kwa afya zao, haswa lishe, elimu, na mengineo mengi.  Si hayo tu, bali watoto wengi hulazimika kulala njaa, kuolewa utotoni na hata kukeketwa.

 

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *