mtoto.news

Mambo Kumi Kuhusu Unyanyasaji wa Watoto

March 20, 2023

Mambo kumi kuntu kuhusu unyanyasaji wa ngono kwa watoto

Unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto kwa bahati mbaya ni mwiko kwenye jamii zetu, na mara nyingi, hakuna anayejadili suala hili licha ya kuenea kwake katika jamii. Walakini, wakati tutakapojitahidi kuleta mwanga kwenye ukweli huu, basi tutaweza kuokoa watoto wengi mno. Tafadhali soma mambo haya kumi, yaliyo na ukweli kuhusu unyanyasaji wa kingono kwa watoto, na ujifunze mwenyewe na watoto wako ili kujua pia jinsi ya kuuzia.

Ukweli 1: Mara nyingi watoto hawaongei wala hawamwelezei yeyote yule kuhusu unyanyasaji wao. 

Kuna sababu kadhaa zinazoelezea kwa nini watoto hawawezi kuongea wakati wanaponyanyaswa kingono, kwani wengi wao huogopa kuingia kwenye matatizo, na wakati mwingine ni mzazi ndiye mnyanyasaji na basi hukosa oa kukimbilia. Pia, wakati mwingine watoto wanaonyanyaswa huwa bado hawajaanza kuongea au wana ulemavu wa kiakili na kimakuzi.

Ukweli wa 2: Hatuwezi Kuwabaini Wanyanyasaji

Kwa bahati mbaya, hakuna rangi au tabaka ambalo ni la kawaida kwa wanyanyasaji, wanafanana na mtu mwingine yeyote na inaweza hata kuwa mtu ambaye anafanya kazi na watoto.

Ukweli wa 3: Ni Vigumu kwa Mtu Aliyenyanyaswa Kijinsia Akiwa Mtoto Kuwa Mnyanyasaji Anapokuwa Mtu Mzima.

Kwa kweli watoto wanaonyanyaswa wana uwezekano mkubwa wa kunyanyaswa hata watakapokuwa watu wazima. Na kwa mara nyingi, wao na hisia za kutokuwa na thamani ambayo inaweza kusababisha wao kuwa wahasiriwa wa matumizi mabaya ya dawa za kulevya, unyanyasaji wa nyumbani au hata biashara ya ngono.

Ukweli wa 4: Unyanyasaji wa Mtoto Hutokea KILA MAHALI

Unyanyasaji wa watoto hutokea katika tabaka zote za kijamii, dini na makabila. Haina mipaka.

Ukweli wa 5: Wanaume na Wanawake Huwanyanyasa Watoto Kijinsia

Ingawa si jambo la kawaida sana, wanawake pia huwanyanyasa watoto, ikijumuisha pale ambapo wanapofunzwa au kulazimishwa kumdhulumu mtoto.

Ukweli wa 6: Waathiriwa Kawaida Huwajua Wanyanyasaji wao 

Zaidi ya asilimia 90 ya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto hufanywa na mtu aliye karibu nao, haswa wale ambao watoto huwaamini.

Ukweli wa 7: Kuna Aina Kadhaa za Unyanyasaji

Kuna aina nyingi za unyanyasaji wa kijinsia kama vile mtu binafsi, genge, kikundi, kupanga mitaani, mtandaoni na rika-kwa-rika. Kujidhulumu pia ni tatizo kubwa, na unyanyasaji kwa faida ya kifedha kama vile utiririshaji wa moja kwa moja mitandaoni.

Ukweli wa 8: Unyanyasaji wa Kijinsia kwa Mtoto Unaweza Kuzuilika

Unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto unaweza kuzuilika, ingawa kujikinga mapema, na kujuwa elimu ya kuzuia unyanyasaji ni muhimu mno.

Ukweli wa 9: Watoto Hawaweza Kusahau Haraka Wakati Wamenyanyaswa  Kijinsia

Watu wazima mara nyingi huathiriwa sana na kiwewe cha utotoni na unyanyasaji. Huwezi tu “kuisahau na kupona”. Walionusurika wanahitaji matibabu na usaidizi sahihi ili kuondokana na athari za unyanyasaji na kiwewe, ndiposa waweze kupona na kuishi maisha kamili na yenye afya.

Ukweli wa 10: Watu Wanaonyanyasa Watoto Kijinsia si Wagonjwa wa Akili kwa Kawaida

Hakuna ushahidi wa watu wanaofanya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto kuwa wagonjwa wa akili. Mara nyingi tunawaona katika nafasi za kuaminiwa, wanatoka sehemu zote za jamii, na wanaweza kuwa katika taaluma mbalimbali.

Je, utafanya nini iwapo mwanao ataamua kukuongelesha kuhusu unyanyasaji aliotendewa?

Mtoto wako akiamua kuongea kuhusu unyanyasaji kwako, NSPCC inatoa ushauri huu wa jinsi ya kujibu:

  1. Sikiliza kwa makini
  2. Wajulishe wamefanya jambo sahihi kwa kukuambia
  3. Waambie sio kosa lao
  4. Usikabiliane na mnyanyasaji
  5. Ripoti kile mtoto wako amekuambia kwa mamlaka husika

Nchini Kenya, unaweza kutuma ujumbe pepe au kupiga kwenye nambari hii : 0729 209 398 / 0800720308 (free) au 0717 968 219 ili uweze kurepoti suala lolote lile kuhusu unyanyasaji wa kingono wa mtoto.

Isitoshe mtoto yeyote yule anaweza kutumia nambari 116 iwapo atahisi au atakuwa ananyanyaswa kingono au kijinsia, ili aweze kurepoti kwa mamlaka husika.

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *