mtoto.news

Pembe ya Afrika- Watoto Zaidi ya Millioni Saba Wamesalia Utapiamlo

May 25, 2023

Mvua imeleta ahueni na matumaini, lakini pia vitisho vipya, na ahueni haitokei kwa haraka, bali huchukua muda ili mazao na mifugo kukua tena

Zaidi ya watoto milioni saba walio chini ya umri wa miaka mitano wamesalia na utapiamlo na wanahitaji msaada wa haraka wa lishe, na zaidi ya wavulana na wasichana milioni 1.9 wako katika hatari ya kufariki kutokana na utapiamlo mkali . Jamii zilizo katika mazingira magumu zimepoteza ng’ombe, mazao, na maisha mengi katika kipindi cha miaka mitatu ya mvua zilizokosa kunyesha.

“Mgogoro katika Maeneo hayo ya Pembeni mwa Afrika umekuwa mbaya kwa watoto. Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, jamii zimelazimika kuchukua hatua kali ili kuishi , huku mamilioni ya watoto na familia wakiacha nyumba zao kutokana na kujizatiti katika kutafuta chakula na maji. Mgogoro huu umewanyima watoto mambo muhimu ya utotoni ikiwemo chakula cha kutosha, nyumba, maji salama, na hata kwenda shule.” alisema Mohamed Fall, Mkurugenzi wa UNICEF wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Matokeo mabaya

Wakati mvua hizo zikiahirisha hali mbaya zaidi, pia zimesababisha mafuriko, kwani ardhi yenye kiu kubwa haiwezi kunyonya maji mengi, na kusababisha watu wengi kuhama, kuwa katikati ya hatari ya magonjwa, upotezaji wa mifugo na uharibifu wa mazao.

Nchini Somalia, mvua hiyo imesababisha mafuriko ambayo yameharibu nyumba, mashamba na barabara, pamoja na kusomba mifugo na kusababisha kufungwa kwa shule na vituo vya afya. Makadirio ya awali yanaonyesha kuwa mafuriko ya ghafla na ya mito kote nchini yameathiri takriban watu 460,470, huku karibu watu 219,000 wakilazimika kuyahama makazi yao hasa katika maeneo yanayokumbwa na mafuriko.

Mafuriko pia yamesababisha uharibifu mkubwa na watu kuhama katika maeneo kadhaa ya Ethiopia. Mafuriko hayo yameongeza hatari ya watu ambao tayari wameathirika zaidi na ukame na kuzidisha hatari za kiafya , ikiwa ni pamoja na kipindupindu, huku mlipuko wa sasa ukiwa miongoni mwa mafuriko marefu zaidi kuwahi kurekodiwa nchini Ethiopia.

“Mvua imeleta ahueni na matumaini, lakini pia vitisho vipya, na ahueni haitokei kwa haraka, bali huchukua muda ili mazao na mifugo kukua tena” alisema Bwana Fall.

Takriban watu milioni 23 wanakabiliwa na viwango vya juu vya uhaba wa chakula nchini Ethiopia, Kenya, na Somalia. Idadi ya watoto walio na utapiamlo mkali wanaotafuta matibabu katika robo ya kwanza ya mwaka huu, hii inasalia kuwa kubwa zaidi kuliko mwaka jana na kuna uwezekano itaendelea kuwa juu kwa muda mrefu.

Juu ya mahitaji ya lishe, hali mbaya ya hewa, ukosefu wa usalama, na uhaba, basi kumekuwa na matokeo mabaya kwa wanawake na watoto, hali ambayo inayozidisha hatari ya unyanyasaji wa kijinsia (GBV), unyonyaji wa kingono na unyanyasaji .

“Mwaka huu, ufadhili zaidi unaobadilika hautasaidia tu watoto kupona kutokana na mzozo wa ukubwa huu, lakini pia utaenda katika kuendeleza mifumo thabiti na endelevu kwa watoto katika kanda, ambayo inaweza kuhimili athari za hali ya hewa na majanga mengine ya siku zijazo,” Bwana Fall alisisitiza haja ya ufadhili zaidi. “Kutokana na hali mbaya ya hewa ambayo tunaiona leo katika Pembe ya Afrika, mgogoro unaofuata unaweza kukumba iwapo bado watoto na familia hawajapata nafasi ya kupona ,” aliongeza.

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *