mtoto.news

Familia Yalilia Haki Baada ya Msichana Kunajisiwa na Genge la Watu 6

May 29, 2023

Yasemekana kwamba, baada ya tukio hilo msichana huyo alilazimishwa kumwaga tindikali kwenye sehemu zake za siri.

Familia moja kutoka Kaunti ya Homa Bay, eneo bunge la Ndhiwa, inatafuta haki kwa binti yao mwenye umri wa miaka 17 anayedaiwa kunajisiwa na kundi la wanaume sita.

Mwathiriwa kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Kaunti ya Homa Bay ambapo alikimbizwa akiwa na majeraha baada ya kisa hicho kilichotokea Jumatatu usiku katika Mji wa Homa Bay. Kulingana na familia yake, msichana huyo aliondoka nyumbani maeneo ya Ndhiwa wiki mbili zilizopita na mamake hakujua alikokwenda.

Msichana huyo alisema kwamba wanaume hao walimkabili alipokuwa akitembea katika Mji wa Homa Bay usiku na kumnajisi karibu na baa.

Baada ya adha hiyo, alisema mmoja wa wanaume hao alijaribu kumlazimisha kumwaga tindikali kwenye sehemu zake za siri, kabla ya wanaume hao kumpeleka sehemu tofauti. Afisa wa watoto katika kaunti ndogo ya Homa Bay Joseph Otieno alisema amepokea habari kuhusu kisa hicho na afisi yake inashirikiana na maafisa wa usalama ili kuwasaka washukiwa hao.

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *