Ujuzi wa lugha zaidi ya moja kwa watoto ni njia mojawapo ya kuwakuza na kuwawezesha kuwasiliana na watu wengi.
Baraza la mawaziri la Uganda, lilipitisha utekelezaji wa kongamano ya East African Community (EAC) hapo tarehe 5 Julai.
Kongamano hilo limekuwa likisisitiza Uganda kupitisha Kiswahili kama lugha ya Taifa, hii ikiwa njia moja ambayo itaweza kuleta uelewano kati ya nchi za Africa mashariki kama vile Kenya,Tanzania, Rwanda, Burundi na DR Congo.
Uelewano huu utawasaidia hususan wanafunzi kwenye masomo, kufanya utafiti na hata kushiriki michezo ya kitaifa.
Aidha, watoto katika shule ya msingi na upili hawaweza kungamua kuwa kuna aina nyingi ya kazi baada ya kujua lugha zaidi ya moja.
Mfano wa kazi hizo ni kama ukalimani, umanju, ualimu, malenga na kadhalika.
Ujuzi wa lugha nyingi, pia husaidia katika kujieleza, kujitetea, kutoa maoni na hata kuelewa jamii za lugha hizi tofauti kwa kina.
Hata hivyo, ujuzu huu wa lugha hutoa changamoto ya kupata kikwazo cha lugha wanapotembea maeneo ambayo wanajamii wanazungumza lugha ya kipekee.
Kulingana na (BBC), watoto hukisiwa kuweza kujifunza lugha haraka kuliko watu wazima. Hii ni kwa sababu watoto huhisi haja ya dharura ya kufahamu lugha ili kuweza kuchangamana na jamii tofauti.
Baadhi ya shule za nchi ya Kenya, lugha ya Ufaransa, Ujerumani, Kiswahili na Kiingereza zimepewa kipaumbele, na hukuzwa kwa wingi.
Hii ni njia bora kwani huweza kuwafanya wanafunzi kukuwa na uwazi wa fikra wanapokua. Pia itawawezesha watoto kupata fursa ya kushiriki katika semina ambazo zitawakuza kitalanta au kimasomo.
By Eddah Waithaka.
Leave a Reply