Mapema Aprili mwaka wa 2023, mchungaji Paul Makenzi wa Good News International mjini Kilifi, alikamatwa na maafisa wa Kurugenzi ya Upelelezi wa Jinai kwa madai ya kuua na kuwazika watoto katika makaburi ya kina kirefu.
Tangia hapo, wachunguzi wameweza kufukua miili iliyopita 110 hadi sasa, huku wengi wao wakiwa watoto. Isitoshe mnamo jumatatu tarehe 1 mwezi Mei, wachunguzi walisema kuwa, tayari wamekamilisha uchunguzi wa miili 10, inayojumuisha watoto tisa wenye umri wa kati ya miezi 18 na miaka 10. Miili ya watoto iliyochunguzwa ilionyesha dalili za njaa na ukukosefu hewa.
Mamlaka yasema kuwa, waliofariki ni waumini wa kanisa la Good News International Church linaloongozwa na mchungaji Paul Mackenzie anayedaiwa kuamuru waumini kufa kwa njaa ili wawe wa kwanza kwenda mbinguni kabla ya mwisho wa dunia.
Kufikia sasa, watu 44 wameokolewa kutoka katika eneo hilo la vifo, huku baadhi yao wakiwa watoto 11, na mmoja wao akiwa mtoto wa wiki mbili, Waziri wa Kazi na Ulinzi wa Jamii Florence Bore alifichua hayo. Isitoshe, waziri huyo alinena kwamba, kwa sasa watoto wote walioweza kuokolewa washaanza kuzoea makazi yao mapya na wanapokea matibabu.
Aidha, Ijumaa iliyopita, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) aliwahusisha Ezekiel Odero wa New Life Prayer Centre na Mackenzie na vifo vya Shakahola.
Mchungaji wa kanisa la Goods News International Paul Mackenzie na New Life Prayer Center na kasisi wa Kanisa hilo Ezekiel Odero wameratibiwa kufikishwa katika Mahakama ya Sheria ya Shanzu hivi leo.
Kasisi Odero alikamatwa Alhamisi iliyopita katika kanisa lake la Mavueni kaunti ya Kilifi na anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Bandari.
Leave a Reply