mtoto.news

Categories
latest latest Latest News OCSEA

Mwanamume Akamatwa kwa Kusambaza Ponografia ya Watoto Kupitia Gmail

Mwanamume mmoja anayeshukiwa kusambaza ponografia ya watoto amekamatwa katika eneo la Majengo, Mombasa.


Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), mshukiwa huyo, Ramadhan Yahya Hussein, mwenye umri wa miaka 26, alikamatwa kufuatia taarifa kutoka Kituo cha Kitaifa cha Watoto Waliopotea na Waliodhalilishwa (NCMEC).

“Hussein amekuwa akisambaza ponografia ya watoto kupitia akaunti yake ya Gmail huku akijihusisha na biashara ya Nyenzo za Unyanyasaji wa Kijinsia kwa Mtoto (CSAM),” ilisomeka sehemu ya ripoti ya DCI.

Baada ya kukamatwa, Hussein aliwaongoza maafisa wa upelelezi hadi nyumbani kwake katika kijiji cha Likoni Maweni, ambako simu mbili za rununu, kadi ya kumbukumbu, na stakabadhi mbalimbali za utambulisho zilipatikana. Vifaa hivyo sasa vinapitia uchunguzi wa kitaalamu ili kupata ushahidi zaidi.

Kwa sasa, Hussein anazuiliwa na polisi akisubiri hatua zaidi za kisheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *