mtoto.news

Watoto Milioni 160 Wako Katika Ajira ya Watoto

June 7, 2022

Ulinzi wa mtoto ni kuwakinga dhidi ya unyonyaji, unyanyasaji, kutelekezwa, vitendo vyenye madhara na ukatili.

Watoto-waathiriwa wa ukatili -waliokaribia milioni 4.4 kutoka nchi 129, ndio walioweza kupata hudama za afya, za kisheria, na za wakaazi wa kijamii.
Aidha, asilimia 25 ya watoto ni walio na miaka chini ya kumi, huku asilimia 41 wakiwa na miaka kati ya kumi hadi kumi na nne, na asilimia 34 wakiwa na miaka kumi na tano, hadi kumi na saba.

Mnamo mwaka wa 2021, baada ya kufungwa kwa shule, pamoja na kukatizwa kwa upatikanaji wa afya, ulinzi wa watoto , na vifo vya walezi vilivyotokana na janga la COVID-19 vimewaweka watoto katika hatari zaidi ya ukiukwaji wa haki kadhaa, kama vile ukatili dhidi yao, Ndoa za utotoni, ajira ya watoto, biashara haramu na utengano baina ya watoto na familia.

Ndani ya miaka miwili, athari hizi za tishio la haki ya ulinzi kwa watoto zimezidi kuvuka mipaka hasa kwa watoto wanaoishi katika nchi zenye hali ngumu mno.

Huku watoto walio katika nchi zilizokumbwa na migogoro ndio walioathiriwa zaidi, kwani miktandha mingine inasitiza vitisho kwa ulinzi wa watoto, Ikiwa ni pamoja na umaskini, kupoteza uhai, vurugu katika njia za uhamiaji, na vurugu mitandaoni.

Watoto pia wanakabiliwa na ubaguzi na kutelekezwa kutokana na ulemavu, ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni, mwelekeo wa kijinsia ,utambulisho wa kijinsia, na ukabila.

Kutokana na hali hii, UNICEF Child Protection, ilifanya kazi pamoja na washirika katika nchi 153 ili kuendeleza maendeleo katika mwaka wa mwisho wa Mpango wa Mkakati wake, 2018–2021. 

UNICEF ilirekebisha programu ili kuendelea kuwafikia watoto walio katika mazingira magumu na waliotengwa kote ulimwenguni, huku ikifikia idadi kubwa ya watoto walio katika maeneo mengi ya kazi ya ulinzi wa watoto ya UNICEF.

Watoto milioni 160 wako katika ajira ya watoto ulimwenguni, hii ni sawa na mtoto mmoja kati ya wakumi duniani.

Ajira ya watoto ni sababu ya matokeo ya umaskini, kuimarisha usawa wa kijamii na ubaguzi. Maendeleo ya Kimataifa dhidi ya ajira ya mtoto imekwama kwa mara ya kwanza ndani ya miongo miwili, huku ikisema kwamba, uondoaji wa ajira ya mtoto ifikapo mwaka wa 2025 hautawezekana.

UNICEF

Vurugu, unyonyaji, watoto kutelekezwa na kunyanyaswa huwaathiri kihisia, kijamii, kiakili na kimwili.
Kwa hivyo, haya yote yanakiuka haki za kimsingi za watoto.

Watoto wanaoishi katika maeneo yenye migogoro na katika mazingira tete wako hatarini.

Na kwa mara nyingi SDGs zinazohusiana na ulinzi wa mtoto, ambazo zimejikita wazi haki za binadamu, hazifuatwi

CECILIA SCHARP, ASSISTANT DIRECTOR GENERAL, SWEDISH INTERNATIONAL DEVELOPMENT COOPERATION AGENCY (SIDA)

Ripoti Kamili ; UNICEF

Mwandishi-Khadija Mbesa

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *