mtoto.news

Serikali Yazindua Elimu ya Ngono ili Kukinga Mimba za Utotoni

June 30, 2022

Serikali imezindua mpango unaolenga kukabiliana na ongezeko la matukio ya mimba za utotoni.

Mpango huo uliopewa jina la Imarisha Msichana utafanyiwa majaribio katika kaunti 20 zilizochaguliwa ambazo zilipatikana kuwa na kesi nyingi zaidi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Evelyne Owuoko mwakilishi wa Waziri wa Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi Julius Jwan, alisema kuwa, shule nane kutoka kaunti zilizochaguliwa zitachukuliwa na kuwa wa kwanza kufaidika na mpango huo.

Mpango huo utaendelea kwa muda wa miaka mitatu, ambayo ni kuanzia Juni, mwaka wa 2022 hadi Juni mwaka wa 2024.

Walengwa wakuu ni akina mama wachanga, au vijana wenye umri wa miaka 9 hadi 18 na wanawake wenye umri wa miaka 19 hadi 25.

Hata hivyo, Owuoko aliwataka washikadau wanaohusika kuwasiliana na Taasisi ya Ukuzaji Mitaala ya Kenya.

Huku akisema kwamba, hii itahakikisha maudhui yanayosambazwa kwa wanafunzi hayatakuwa na athari yoyote mbaya.

“Elimu ya ngono ni nyeti sana kwa hivyo tunahitaji kujua nini cha kuwaambia wasichana hawa ili kusiwe na taarifa za kupotosha zinazotolewa kwao,” Owuoko alisema.

Akisoma hotuba ya Jwan, Owuoko alikiri changamoto zinazokabili vita vya kukabiliana na mimba za utotoni.

Owuoko ambaye anahudumu kama mkurugenzi wa mipango na ushirikiano katika Wizara ya Elimu, alibainisha kuwa serikali imeweka mikakati kadhaa ya kukabiliana na changamoto hizi.

“Nyingi ya changamoto hizi husababishwa na kushindwa kutekeleza stadi za maisha ambazo ni muhimu katika maisha ya watoto hawa,” alisema.

“Inawezekana na imethibitishwa kwamba, mzazi mchanga anaweza kurejea kwenye masomo yake na pia kufaulu kwenye masomo hayo,” Otieno alisema.

Msichana kupata ujauzito akiwa mchanga, haimaanishi kwamba masomo yake yashakatika bali anaweza kuendelea na masomo yake na akafaulu katika maisha yake ya baadae.

Kaunti zilizochaguliwa ni Nakuru, Nairobi, Machakos, Elgeyo Marakwet, Kiambu, Garissa, Bungoma, Kakamega, Nyeri, na Migori,

Nyingine ni Murang’a, Kajiado, Narok, Homa-Bay, Trans-Nzoia, Nyandarua, Busia, Meru, Siaya, na Turkana.

Katika mfumo wa programu hii, wasichana wadogo watapewa ujuzi muhimu ili waweze kuvuka kikamilifu kutoka ujana wao hadi utu uzima.

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *