mtoto.news

Ukeketaji na Ndoa za Mapema Zashika Kasi

June 30, 2022

Wasichana walio na umri wa miaka kumi na miwili wanalazimishwa kuolewa na kukeketwa (FGM) haswa katika Pembe ya Afrika, huku ukame mkali zaidi katika kipindi cha miaka arobaini ukisukuma familia ukingoni.

 Idadi kubwa ya watoto wako katika hatari ya kuacha shule nchini Ethiopia, Kenya na Somalia, hii ni kutokana na athari za Ukame n.k.

Familia nyingi kutoka Pembe ya Afrika, zakabiliwa na chaguo la kustahimili hali ya ukame, unaochochewa na mabadiliko ya hali ya hewa, huku vyanzo vya maji vikikauka, na kuua mifugo, na tukiongeza athari kubwa ya vita nchini Ukraine ambayo inazidisha kupanda kwa bei ya vyakula na mafuta.

Zaidi ya watoto milioni 1.8 wanahitaji mno matibabu kutokana na utapiamlo mkali unaotishia maisha katika eneo hilo, huku watu 213,000 sasa wakihukumiwa kuwa katika hatari ya njaa nchini Somalia.

Kulingana na Famine Early Warning Network Idadi inayoongezeka ni ya wazazi au walezi ambao wanawaozesha wasichana wao ili wapate mahari ndiposa waweze kusaidia familia nzima.

“Tunaona viwango vya kutisha vya ndoa za utotoni na ukeketaji katika Pembe ya Afrika – huku baadhi ya familia maskini zikipanga kuwaoza wasichana wenye umri wa miaka kumi na mbili kwa wanaume walio na zaidi ya mara tano ya umri wao,”

Ndoa za utotoni na ukeketaji humaliza maisha ya watoto, kwani huwafukuza wasichana shuleni na kuwaacha katika hatari zaidi ya unyanyasaji wa nyumbani na umaskini. Takwimu tulizonazo hazielezi ukubwa wa tatizo kwani maeneo makubwa ya Pembe ya Afrika hayana vifaa maalum ambapo kesi zinaweza kuripotiwa.

ANDY BROOKS, MSHAURI WA ULINZI WA MTOTO WA UNICEF KATIKA KANDA. MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA.

Kulingana na UNICEF, Wasichana Nchini Kenya pia wanakabiliwa na hatari kubwa ya ndoa za utotoni na ukeketaji. 

Kaunti 14 kati ya 23 zilizoathiriwa na ukame tayari ni maeneo yenye ukeketaji, huku viwango vya maambukizi vikiwa hadi asilimia 98. 

Wasichana katika maeneo haya sasa wako katika hatari ya kukeketwa wakiwa na umri mdogo, huku familia zikiwatayarisha kwa ndoa. 

Pia kuna ripoti za wasichana wanaoishi katika mikoa ya mpakani kupelekwa nchi jirani kufanyiwa ukeketaji, au kuolewa na wanaume wazee katika nchi jirani, ambapo viwango vya ukeketaji vinaweza kuwa juu zaidi. 

Katika kanda nzima, wanawake na wasichana katika maeneo yaliyoathiriwa na ukame wanalazimika kutembea umbali mrefu kupata maji na rasilimali nyingine za kimsingi, na kuwaacha katika hatari ya ukatili wa kijinsia. 

UNICEF yatoa wito kwa huduma za kushughulikia ulinzi wa watoto kutokana na Ukeketaji na Ndoa za mapema kuongezwa kwa haraka.

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *