mtoto.news

Elimu Sawa kwa Jinsia Zote

July 22, 2022

Kutokana na utafiti wa hivi karibuni, wasichana asilimia 76 ndio walio na fursa ya kupata elimu ikilinganishwa na asilimia 88 ya wavulana ambao hupata fursa hiyo.

Kulingana na UNICEF, umaskini ndio sababu kuu inayofanya wasichana kukosa elimu. Kwa sababu hii, wazazi wanakosa kuwapeleka watoto wao hususan wasichana shuleni iwapo hawana karo.

Aidha, umaskini huu pia unawafanya wasichana kukosa kuenda shule kwa sababu ya kukosa pesa za kununua sodo.

Katika nchi ya Kenya, baadhi ya jamii mbalimbali bado hawaamini kuwa kuna manufaa yoyote ya wasichana wadogo kuelimishwa.

Hii ni kwa sababu wanaamini kuwa wasichana wadogo wakipelekwa shuleni familia haitaweza kupata mahari. Hii ni kutokana na kuwa, wanaume hawa wanao waoa wasichana hawa wadogo hawapendi kuoa wasichana ambao wameenda shuleni kwa sababu wanajua mambo mengi.

Duniani, wasichana milioni 12 walio chini ya umri wa miaka18 huozwa kila mwaka.

Kusomesha watoto wa kike ina manufaa kwa sababu wanapokuwa wakubwa, wataweza kupata watoto walio na afya nzuri. Hii pia itawezesha kuvunja mzunguko wa kutojua kusoma na kuandika na pia umaskini.

Serikali, mashirika ya elimu, wanaharakati na haiba wa kimataifa wanafaa kuingilia kati Ili kuwezesha wasichana wadogo kupata elimu sawa na wavulana wenzao.

Tohara kwa wasichana wadogo pamoja na ndoa za kimapema zinafaa kumalizwa Ili kuwezesha elimu bora kwa wasichana.

Serikali pia inafaa kusambaza sodo katika shule na vijiji Ili kusaidia wasichana kuenda shuleni.

Zaidi ya hayo, ili kuwezesha malengo ya maendeleo endelevu kufika, elimu kati ya wasichana na wavulana inafaa kuwa sawa.

By Eddah Waithaka

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *