mtoto.news

Magoha Abadilisha Tarehe ya Kufungua Shule

August 13, 2022

Waziri wa Elimu George Magoha ametangaza kwamba tarehe ya kufunguliwa kwa shule imebadilishwa kutoka Jumatatu 15 hadi Alhamisi 18, 2022.

Katika taarifa yake Jumamosi, Agosti 13, Magoha alieleza kuwa kutokana na zoezi linaloendelea la kujumlisha kura, serikali imeazimia kusogeza tarehe ya kufungua tena.

Aliwataka wadau wote kuivumilia serikali wanaposhughulikia suala tata la kujumlisha kura.

Kufuatia mwenendo wa Uchaguzi wetu wa Kitaifa mnamo Jumanne, Agosti 9, 2022, shughuli ya kujumlisha kura bado inaendelea. 

“Kwa hiyo, kufuatia mashauriano zaidi, nawasilisha uamuzi wa Serikali kuhusu kusitishwa kwa ufunguaji upya wa vyuo ZOTE vya Elimu ya Msingi kuanzia Jumatatu, Agosti 15, 2022 hadi Alhamisi, Agosti 18, 2022,” ilisomeka taarifa hiyo.

Waziri huyo aliomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza kutokana na kubadilishwa huko kwa tarehe ya kufungua shule.

 

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *