mtoto.news

Hofu ya Usalama wa Watoto Baada ya Matokeo ya Uchaguzi Kutangazwa

August 16, 2022

Wazazi wamesema kuwa, huenda wasiwaachilie watoto wao warudi shuleni hadi watakapohakikishiwa kuwa, hali ya kisiasa ipo salama kwa wanafunzi.

Mwenyekiti wa chama cha wazazi wa kitaifa Nicholas Maiyo alisema kuwa ingawa wazazi walipongeza uamuzi wa kuahirishwa siku ya kufunguliwa kwa shule hadi Alhamisi wiki hii, hali ya usalama wa kisiasa ni muhimu mno, kwani hawawezi kuwaruhusu watoto kurudi shule iwapo kutakuwa na tahfash.

Kila mwananchi anafaa kudumisha amani nchini, haswa wakati huu ambapo cheche za chuki zinasambazwa mitandaoni, mitaani na hata majumbani, hii ni baada ya matokeo ya Rais Mchaguliwa kutangazwa.

Watoto wengi wameonekana wakijiunga na vikundi vya kusherehekea, na wengine wakijiunga na vikundi ya kupinga matokeo hayo. Jambo ambalo linatishia usalama wa watoto, kwani mara nyingi vikundi hivi huwa na vurugu.

Ni wajibu wa kila mzazi au mlezi kuhakikisha kuwa watoto wao wako salama na wanakemewa kutokana na kujiunga na makundi haya.

Aidha, Baadhi ya wazazi mjini Mombasa watalazimika kulipa Sh300 za ziada ili kubadilisha tarehe ya kusafiri kwa watoto wao kurudi shuleni, hii ni baada ya Waziri George Magoha kuahirisha tarehe ya kufungua shule hadi Agosti 18.

 

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *