Ukiukaji wa haki za watoto umeendelea kuwa tishio sugu. Hii imeonyeshwa na shirika la WHO ambayo inasema kuwa kimataifa, inakadiriwa kuwa watoto milioni moja kutoka miaka miwili hadi kumi na saba ndio wamepitia ukiukaji wa haki kimwili, kihisia na pia kingono. https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/violence-against-children
Nchini Kenya, ukiukaji wa haki za watoto hususan hutokea nyumbani, shuleni na pia katika jamii wanamoishi.
Hii inaonyeshwa na vile watoto wadogo hufanyishwa kazi ngumu bila kupewa malipo yoyote. Kazi hizi mara nyingi huwa katika mashamba kubwa ambapo watoto hawa huweza kutumiwa kulima au kuvuna. Kulingana na shirika la UNICEF, karibu watoto asilimia saba katika umri wa tano hadi kumi na saba, wamehusishwa katika fomu za ukiukaji wa haki kama vile kuajiriwa bila malipo na pia watoto wengine kuajiriwa katika maeneo iliyo na hatari za kiafya.
Maeneo haya yanaweza kuwa viwanda ambavyo zinatengeneza kemikali hatari au zinatoa hewa iliyo hatari kwa mwili au pia mashamba ya kupalilia. https://data.unicef.org/topic/child-protection/child-labour/
Ukiukaji wa haki za watoto huleta madhara kama vile majeraha kali kwa watoto, udhoofishaji wa kiafya, mimba za mapema kwa wasichana, vifo na pia kuharibu fursa yao ya kupata maisha bora baadaye.
Aidha, watoto walemavu pia hupitia ukiukaji wa haki kwa kubaguliwa, kutengwa na kunyanyapaliwa. Hii huwafanya kupoteza tumaini na maisha ya kuweza kufanya bora wanapokuwa wakubwa.
Wazazi, walezi, serikali na pia haiba wa kimataifa wanafaa kuingilia kati katika kutetea haki za watoto. Kila mtoto ana uhuru na haki kutokana na unyanyasaji na ukiukaji wa haki zao.
Leave a Reply