mtoto.news

Hatua Za Kuhakikisha Usalama wa Watoto walio Katika Jamii Zilizoathiriwa na Hali ya Hewa.

August 22, 2022

Je ni jinsi gani mabadiliko ya hali ya hewa huchochea ukatili dhidi ya watoto?

Takriban watoto bilioni moja walio na umri wa miaka 2-17 huathiriwa na ukatili wa kimwili, kingono, au kihisia kila mwaka.

mabadiliko ya hali ya hewa huongezeka wakati wa ukame na uhaba wa maji, mafuriko, na hata kuongezeka kwa joto huku ikiathiri watoto upande wa uhamiaji, migogoro, umaskini na ukosefu wa chakula, afya ya kisaikolojia na dhiki.

Haya yanaongeza matukio ya ukatili dhidi ya watoto, kama vile ajira za utotoni, ndoa za utotoni, unyanyasaji wa kijinsia, unyanyasaji wa kimwili, ukatili wa kijinsia, kutelekezwa, biashara haramu ya binadamu na masuala ya afya ya akili.

Kuna hatua kadhaa zinazofaa kuchukuliwa ili kuhakikisha watoto kutoka  jamii zilizoathiriwa na hali ya hewa wako salama.

Hatua ya Kwanza-Kila mtu anafaa kukubali kwamba, mabadiliko ya hali ya hewa yanaongeza viwango vya ukatili dhidi ya watoto.

Utafiti ulioibuka umegundua kuwa mabadiliko ya hali ya hewa huchangia vurugu za moja kwa moja na za kimuundo, ikiwa ni pamoja na ukatili dhidi ya watoto.

Hatua ya Pili-Hatuna budi ila kuimarisha uzuiaji wa ukatili dhidi ya watoto kwa njia ya kujikimu kimaisha; kushughulikia kanuni za kijamii na kuendeleza programu za shule.

Mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kuathiri ustawi kwa njia tofauti katika kila hatua ya maisha ya mtoto kama vile ukosaji wa virutubisho kwa watoto walio chini ya miaka 5, hadi kuondolewa kwa elimu ili kuchangia mapato ya kaya kwa watoto wa miaka 5-18.

Mfano unaweza kuonekana katika kisa cha Dugda, Ethiopia, ambapo kuendelea kwa kasi kwa ukame kunaathiri fursa za maisha, kilimo, na mifumo ya chakula, na kusababisha kaya kutumbukia kwenye umaskini wa kupindukia..

Na mara nyingi mno familia zilizo katika hali hii hutumia ajira ya watoto na ndoa za mapema, na uhamiaji usio na usalama kama suluhu ya kuwapa nafuu.

Hatua ya Tatu-Tuimarishe huduma za uzuiaji na mwitikio wa haraka ili kujumuisha ongezeko la hatari ya ukatili dhidi ya watoto, na kukuza hatua zinazotarajiwa.

Kwa mfano, shule zilizo katika maeneo yanayokumbwa na maafa zinaweza kufanya kazi na mashirika ya jamii na mamlaka ili kupanga uanzishaji wa maeneo salama yanayowalenga watoto wakati wa maafa. 

Nafasi kama hizo hutoa msaada wa kisaikolojia na huduma za ulinzi wa watoto kwa watoto.

Serikali za mitaa zinaweza kuanzisha mafunzo ya kuongeza na kuandaa mipango na huduma za ulinzi wa watoto katika jamii, au kuanzisha utangulizi wa mapema wa chakula shuleni.

Mipango kama hii inaweza kusaidia kuwaweka watoto shuleni na kuzuia ajira na uhamaji wa watoto.

Uhamisho wa fedha, ambao mara nyingi hutumiwa katika mwito wa  kibinadamu, unaweza pia kuwa na ufanisi katika programu zote mbili za maendeleo na hatua za kutarajia.

Kiasi kidogo cha pesa kinachotolewa kwa kaya zilizo hatarini zaidi kabla ya hatari inaweza kuruhusu familia kuwa tayari kwa maafa, ambayo inaweza kupunguza mfadhaiko wa kaya.

Hatua ya Nne-Tunafaa Kuwasikiliza, kuwashirikisha na kuwasaidia watoto na vijana katika kupanga na kutafuta suluhisho la kukomesha ukatili dhidi ya watoto,haswa wakati hali ya hewa inabadilika.

Mara nyingi watoto huona misiba ya asili kama aina ya maafa inayowaacha hatarini kwa kutishia au kuharibu nyumba zao, kukatiza maisha yao ya kila siku, na kuweka mafadhaiko katika familia na jamii zao.

Athari hizi za kihisia za mabadiliko ya hali ya hewa kwa watoto na vijana zinaweza kuunganishwa na majibu yasiyoridhisha ya serikali kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa.

Wazazi na walimu wanafaa kuwa na mwongozo kuhusu jinsi ya kuzungumza na watoto na vijana kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, na watu wazima wanapaswa kuona majadiliano kama fursa ya kuwasaidia watoto na kuorodhesha mawazo yao kwa ajili ya hatua chanya za kusaidia kukabiliana na kukomesha mabadiliko ya hali ya hewa, na kushughulikia maafa mengine ya mazingira.

Kupitia hili, watoto na watu wazima wanaweza pia kujifunza thamani ya kujitegemea na umuhimu wa hatua ya hali ya hewa.

Ripoti hiyo ya Barnfonden ilitamatisha ikisema kwamba, watoto, familia, jamii na serikali za mitaa zinafaa kuwa tayari kukabiliana na ongezeko la athari za mabadiliko ya hali ya hewa, kupitia mikakati mbalimbali ya kukabiliana na mabadiliko yahali ya hewa, mikakati na mipango ya kupunguza hatari za maafa, na kuongeza elimu na uelewa wa jinsi ya kuandaa na kuzuia athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa ukatili dhidi ya watoto.

 

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *