mtoto.news

Hadithi za kiafrika zisomwe shuleni.

September 1, 2022

Watoto wafrika wamelelewa katika jamii ambayo imejaa mila na utamaduni wa kimagharibi. Mara nyingi, vitabu na filamu za kiafrika ni chache katika jamii zikilinganishwa na zile za wazungu.

Hii ni changamoto kubwa kwa sababu watoto wakiafrika hukuwa wakiiga tabia za kimagharibi. Hivyo kufanya mila na utamaduni wa kiafrika kudidimia au kutokuwa na maana.

Licha ya hayo, ni vyema kuwa serikali imeweka somo za Kiswahili na kiingereza. Somo hizi zinasaidia mno hususan shule ya upili. Hii ni kwa sababu kuna hadithi fupi na riwaya ambazo husomwa katika somo hizi. Vitabu hizi mara nyingi huwa zimeandikwa na waandishi waafrika wakirejelea wahusika, maeneo na mawazo ya kiafrika.

Ingawa hadithi hizi husomwa tu shuleni, kuna vitabu nyingi ambazo zimeandikwa kuhusiana na wahusika, mawazo, viwango na maeneo ya kiafrika. Mifano ya vitabu hizi ni kama ‘Wangu Wa Makeri the Muranga chieftess,’ ‘Shaka Zulu, ‘ ‘The extraordinary life of Nelson Mandela,’ ‘Queen Nzinga of Ndongo and Matamba,’ ‘The river and the source’ and ‘ Cleopatra.’

Pia kunafaa kuwa na uongezeko wa filamu na katuni za kiafrika. Ni vyema kuwa baadhi ya filamu kama ‘ black panther,’ ‘ wakanda’ na ’12 years of slave’ zimeweza kuenea duniani. Hii inaonyesha kuwa filamu za kiafrika pia zinaweza kuongoza na kila jamii duniani kujua na kuelewa utamaduni na mila za waafrika.

Serikali, walimu na wazazi wanafaa kuwahimiza watoto kusoma hadithi na riwaya za kiafrika. Hii ni Ili kuwasaidia watoto kukua katika mandhari na jamii ya mila na utamaduni zao.Hivi karibuni, watengenezaji wa chokoleti Cadbury waliwaita waandishi wakiafrika kutuma hadithi ambazo walichapisha katika mitandao zao. Hii ni mfano mzuri wakuikuza jamii, mila na utamaduni wakiafrika.

 

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *