mtoto.news

Ni Ipi Hatima ya CBC Baada ya William Ruto Kuapishwa?

September 14, 2022

Rais wa Kenya anayeondoka Uhuru Kenyatta akisalimiana na Rais William Ruto katika Kituo cha Michezo cha Kimataifa cha Moi, Kasarani jijini Nairobi, Kenya, Septemba 13, 2022 wakati wa hafla ya kuapishwa.

Hatima ya Mtaala Unaozingatia Umahiri (CBC) sasa iko kwenye jopokazi litakaloanzishwa wiki ijayo na Rais mpya William Ruto ambaye alichukua uongozi Jumanne.

Ruto alisema kwamba, ataunda Kikosi maalum ili kubaini utendakazi wa mpango huo uliozinduliwa na mtangulizi wake Uhuru Kenyatta mnamo 2018.

Mpango huo umekosolewa vikali na washikadau ambao walishutumu utawala wa Kenyatta kwa kukosa kuwashirikisha katika uundaji wake.

Mfumo huu uliundwa kuchukua nafasi ya mtaala wa 8-4-4.

“Kuna mazungumzo mazito kuhusu elimu na haswa utekelezaji wa mtaala wa CBC. Ushirikishwaji wa umma ni muhimu katika suala hili na nitaanzisha jopokazi la kurekebisha elimu ambalo litazinduliwa wiki zijazo,” Rais Ruto alisema.

“Kuna wasiwasi mkuu kutoka kwa wazazi hasa juu ya mpito pacha wa darasa la mwisho la 8-4-4 na darasa la kwanza la CBC Januari mwaka ujao. Ninawahakikishia wote kuwa kutakuwa na suluhu juu ya suala hilo kabla ya wakati huo,” Rais alisema.

Hata hivyo, ingekuwa bora zaidi iwapo watoto watashauriwa juu ya suala hilo kwani Watoto ndio washikadau wakubwa katika mageuzi yoyote ya Elimu na ndio watakaoathirika zaidi.

 

Ruto alitangazwa mshindi wa kinyang’anyiro cha Urais mnamo Agosti 15, hii ni baada ya kumshinda kiongozi wa muda mrefu wa Upinzani Raila Odinga.

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *