mtoto.news

Akamatwa baada ya miili ya watoto wawili kupatikana kwenye masanduku

September 15, 2022

Polisi  Nchini New Zealand wameripoti kwamba, mwanamke mmoja nchini Korea Kusini ameshtakiwa kwa mauaji ya watoto wawili ambao miili yao ilipatikana kwenye masanduku mwezi uliopita.

Katika kisa kilichoshtua nchi, mabaki hayo yaligunduliwa na watu wasiowafahamu ambao walinunua masanduku hayo kutoka kwa kitengo cha kuhifadhi huko Auckland.

Miili hiyo ilikuwa imehifadhiwa kwa miaka kadhaa. Polisi wanasema waathiriwa walikuwa na umri wa kati ya miaka mitano na 10.

New Zealand imetuma maombi ya kurejeshwa kwa mwanamke huyo kutoka Korea Kusini.

Polisi wamesema kuwa wamefanya kazi kwa karibu na mamlaka ya Korea Kusini katika muda wa wiki tatu zilizopita katika kumsaka mwanamke huyo.

Majina ya watoto hao wawili hayajawekwa wazi.

 

“Kuweza kumweka mtu kizuizini aliye ng’ambo, ndani ya muda mfupi kama huu ni kutokana na ushirikiano na usaidizi wa mamlaka ya Korea na uratibu wa wafanyakazi wetu wa Polisi wa NZ,” Inspekta wa Upelelezi Tofilau Fa’amanuia Vaaelua alisema.

Alisema kwamba, mwanamke huyo alikamatwa na polisi wa Korea Kusini Alhamisi asubuhi.

Aliongeza kuwa umma umetoa “msaada mkubwa” kwa operesheni ya polisi.

Vyombo vya habari vya eneo hilo vimeripoti kuwa mshukiwa anaaminika kuwa na uhusiano na watoto hao. Walisema familia hiyo iliishi Auckland kwa miaka michache na baba wa watoto hao alifariki kabla ya vifo vyao.

Polisi walisema familia iliyopata miili hiyo ilikuwa imetembelea sehemu ya kuhifadhia na kununua trela ya mizigo, ikiwa ni pamoja na masanduku, mapema Agosti.

Kulingana na Daily Mail  Watoto hao wamekuwa wafu kwa miaka minne sasa kabla ya familia hio kununua makabati hayo kutoka kwa mnada Nchini New Zealand.

Maafisa walisisitiza kwamba, familia hiyo haikuwa na uhusiano wowote na vifo hivyo na ilikuwa imeteseka sana katika kipindi kilichofuata ugunduzi huo.

 

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *