mtoto.news

Ruto Ahimiza Juhudi Zilizojumuishwa ili Kupunguza Athari za Mabadiliko ya Hali ya Hewa.

September 22, 2022

Septemba 21st 2022: Rais William Ruto atoa hotuba yake ya kwanza kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.

Mabadiliko ya hali ya hewa nchini Kenya yanaendelea kuwaathiri watoto huku wengi wao wakikabiliwa na utapiamlo mkali unaohitaji matibabu ya haraka.

Akiongea wakati wa hotuba yake kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko New York, Mheshimiwa William Ruto aligusia jinsi maisha ya wananchi yamezorota, haswa baada ya Covid-19 na jinsi mabadiliko ya hali ya hewa yanaharibu uchumi wa sio Kenya tu, bali ulimwenguni kote.

Hali ambayo inasababisha mamilioni ya watu, ikiwemo watoto kutaabika na umaskini, ukosefu wa chakula, maji masafi na mengineo.

“Ustawi wa binadamu uko kwenye tishio kubwa. Sayari yahitaji uangalifu wa haraka. Shinikizo kubwa linaloletwa na vitisho vya kawaida kama vile mabadiliko ya hali ya hewa, shida ya chakula duniani, ugaidi, uhalifu wa mtandaoni, na migogoro ya silaha imechangiwa na usumbufu mkubwa usio na kifani kutokana na Covid-19.”

Mheshimiwa Ruto alisema kuwa maeneo ya ASAL(Ardhi Kame na Nusu Kame) nchini Kenya yameathiriwa sana na mabadiliko ya hali ya hewa kwani mawimbi ya joto yamesababisha vyanzo vya mito na maji kukauka.

Aidha, Ruto amesema kuwa, uhaba wa mvua katika misimu mitatu mfululizo umewaacha wakazi milioni 3.1 wanaoishi katika maeneo ya ASAL kukumbwa na uhaba wa chakula, uhaba wa maji na njaa iliyopita mioaka kutokana na kupanda kwa bei ya vyakula.

“Wakazi milioni 3.1 wa maeneo haya ya ASAL sasa wana uhaba mkubwa wa chakula kwa ulioletwa na uhaba wa mvua katika misimu mitatu mfululizo, iliyosababisha mazao na malisho duni.

Mkusanyiko huu usio na kifani wa matukio mabaya umezidisha uhaba wa maji na njaa na kupanda kwa bei ya vyakula, hii ikikusudia kutatiza ramani ya Kenya katika kuelekea kuwasilisha maisha bora kwa wananchi, huku ikizuia maendeleo ya kufikia SDG 6 na SDG 2.”

Isitoshe, Rais alidosea kwamba vita vya Urusi na Ukraine vimeathiri mfumuko wa bei huku watu wengi wakiachwa bila chakula wala mahitaji ya kimsingi.

Rais William ameipongeza nchi ya Kenya kwa kukomesha uchafuzi wa plastiki, huku akitoa wito kwa wanachama wa jimbo kuunga mkono suala hili na kufanya kazi kwa karibu ili kukabiliana na Mabadiliko ya hali ya hewa.

“Ni ishara tosha kwamba ulimwengu umejitayarisha na kuhamasishwa kuchukua hatua katika kukabiliana na tishio la mabadiliko ya hali ya hewa, baada ya azimio muhimu la kukomesha uchafuzi wa plastiki  kutekelezwa Nchini Kenya. Aidha Kenya imejitolea kufanya kazi kwa karibu na mataifa mengine ili kufuata vyombo vinavyofunga kisheria vinavyolenga kukomesha uchafuzi wa plastiki.” Alisema Mheshimiwa William Ruto.

Nchi nyingi sasa zinashuhudia hali mbaya ya mito, mifereji, na hifadhi za maji ambazo zinakauka kwa sababu ya ukame na mawimbi ya joto yanayosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa. 

Nyanda za kaskazini na nyanda za ASAL za nchi ya Kenya zimeathiriwa sana na ukame ambao ukali wake haujashuhudiwa kwa miaka 40.

“Ripoti ya hivi punde ya Jopo la Serikali Mbalimbali kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (IPCC) inatukumbusha kwamba hatuwezi kumudu kupoteza wakati mwingine kwa mijadala kwani hivi karibuni tutachelewa mno katika kubadili mwendo wa matukio. Sisi kama viongozi, kila siku ni fursa ya kuharakisha juhudi zetu za kukabiliana na mzozo wa sayari tatu.

Hata hivyo, Rais Wiliam Ruto, aliipa kipaumbele sekta ya kilimo, huku akisema kwamba, teknolojia ya kisasa ya kilimo ni njia muafaka kabisa katika kukabiliana na changamoto za mazingira.

“Waheshimiwa, sekta ya kilimo ina mchango kubwa katika kupunguza makali ya mabadiliko ya hali ya hewa. 

Kupitia vipimo mbalimbali vya mazingira, ni ukweli kwamba idadi ya mazoea yana athari chanya au hasi. Kwa hivyo kuwekeza katika teknolojia ya kisasa ya kilimo ni njia moja muhimu ya kukabiliana na changamoto za mazingira.”

Rais William Ruto pia aliwataka wanachama wa jimbo na washikadau wote husika kuonyesha nia thabiti ya kisiasa na kuonyesha ushirikiano mwafaka kwa kusaidia nchi zilizoathiriwa zaidi kifedha na pia kuungana ili waweze kukabiliana na hali ya hewa.

“Ukame mkali umeathiri sio tu eneo la Pembe ya Afrika na maeneo ya Sahel, bali unaendelea kuharibu maeneo mengine mengi, ikiwemo Asia, Ulaya, na Amerika. 

Kwa kuzingatia hili, natoa wito kwa wanachama wa jimbo  na washikadau wote wanaohusika kuonyesha nia thabiti ya kisiasa na kuonyesha ushirikiano wa ufanisi kwa kusaidia nchi zilizoathirika zaidi kifedha, na pia kuweza kugawana teknolojia ya kukabiliana na hali ya hewa”

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *