mtoto.news

Utahakikishaje kuwa talaka haiathiri maisha ya mtoto wako?

September 26, 2022

Ni vipi utahakikisha kuwa talaka yako haimwathiri mtoto wako?

Kulingana na utafiti watu wanne kati ya elfu ulimwenguni waliofunga ndoa wamepitia talaka, na mara nyingi talaka hizi huathiri watoto.

Athari za talaka kwa watoto ni nyingi mno, ila utajitahidi vipi katika kuhakikisha kuwa talaka haitamwathiri mtoto wako?

La kwanza kabisa, ni kujizatiti katika kutowaangazia watoto kwenye mapigano yasiyoisha, au vita vya chuki vilopita mpaka.

Kwa hivyo wewe na mpenzi wako wa zamani mnapaswa kujaribu kuweka tofauti zenu kando na kushirikiana ili nyote wawili muwe na uvutano thabiti na chanya katika maisha ya watoto wenu.

Jaribu kuwasiliana kuhusu mambo kama vile matukio ya shule na kadhalika. Wekeza vitu kama vile siku za kuzaliwa na likizo maalum, na uepuke kushindana juu ya nani anaweza kufanya likizo hio iwe ya kusisimua zaidi, au nani ana uwezo wa kununua zawadi iliyo bora zaidi.

Watoto wengi huamini kuwa, talaka ya mzazi wao imetokana na kosa lao, kwa hivyo jitahidi hakikisha kwamba watoto wako wanajua kwamba hawakuhusika au kusababisha talaka hiyo.

Ni vizuri kuzungumza na watoto wenu mara kwa mara, huku mkiwaelezea kuwa bado mnawapenda na nyote wawili mtajitahidi katika kuboresha maisha yao ya sasa hivi, na ya baadae.

Hakikisha kwamba nyote wawili mnahusika kwenye maisha ya watoto wenu kivyovyote vile, ikiwemo masuala ya shule, mahitaji ya kimsingi na mengineo.

Mara nyingi wazazi hupuuza athari za talaka kwa watoto wao, wakitupilia mbali uwepo wa kiwewe cha saikolojia kwa watoto hawa katika maisha yao ya baadae.

Wazazi wote wawili ni waendeshaji wakuu wa maisha ya mtoto iwapo wataamua kutalikiana.

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *