mtoto.news

Sudan: Mafuriko, mashambulizi ya wanamgambo na njaa yatatiza masomo ya watoto

October 5, 2022

Mafuriko, uvamizi wa wanamgambo na njaa yamesababisha thuluthi moja ya watoto kutupilia mbali shule, huku wengine wakiwa na walimu wachache. Picha: Ashraf Shazly

Kufuatia mvua kubwa na mafuriko nchini Sudan, makumi ya maelfu ya nyumba, visima na mashamba ya kilimo yameharibiwa huku familia 80,000 zikihitaji msaada wa kibinadamu makadirio ya Hilali Nyekundu ya Sudan (SRCS).

Mashirika ya misaada yameonya kwamba, takriban kila mtoto aliye na umri wa kwenda shule nchini Sudan anakosa elimu,

Baadhi ya majimbo nchini Sudan, yalifungua shule baada ya kuchelewa kuzifungua kutokana na mafuriko ya kuvuka mipaka, hii ikiwalazimu watoto wengi kutohudhuria.

Umaskini, ukosefu wa walimu waliohitimu na migomo ya walimu , historia ya janga la Covid-19 na viwango vya chini vya chanjo ni miongoni mwa mambo mengi ambayo yamechangia mgogoro huo.

Kulingana na wizara ya elimu, mafuriko na mashambulizi ya wanamgambo yameharibu zaidi ya shule 600 mnamo Agosti na Septemba. 

kulingana na taarifa ya pamoja ya Unicef ​​na Save the Children, takriban watoto milioni 7 kutoka Sudan wenye umri wa kati ya miaka sita na 18  hawaendi shuleni kabisa.

Jimbo lililoathiriwa zaidi ni Darfur ya kati, ambapo asilimia 63 ya watoto hawaendi shule.

Isitoshe kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, ukame na umaskini,  watoto wengi kutoka Afrika mashariki wamelazimika kuwacha shule kabisa, huku wengi wao, hasa watoto wa kike, wakilazimishwa ndoa za mapema.

 

 

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *