mtoto.news

Data ya MoH : Kiwango cha vifo vya watoto wachanga kimepungua

November 15, 2022

Data kutoka Wizara ya Afya imeonyesha kuwa, Kenya imepata mafanikio makubwa katika kupunguza vifo vya watoto katika miaka 10 iliyopita.

Kumekuwa na upungufu kwa asilimia 30 kwa idadi ya watoto wanaokufa kabla ya kufikisha miaka mitano.

Hii imechangiwa na kuongezeka kwa unywaji wa ORS na Zinki kwa ajili ya udhibiti wa kuhara kwa watoto walio chini ya miaka mitano na kuboreshwa kwa unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee.

Kuanzishwa kwa chanjo mpya za utotoni kama vile pneumococcal na rotavirus, matumizi ya vyandarua vilivyotiwa dawa na kuongeza wakunga wenye ujuzi ni mambo mengine yaliyochangia hayo.

“Ingawa chanjo na juhudi zingine za kuzuia zinapunguza mzigo wa ugonjwa huo, kazi zaidi bado inahitajika,” Waziri wa Afya Susan Wafula alisema.

“Wale wanaoishi katika jamii maskini wako katika hatari kubwa zaidi ya nimonia. Kila mtoto, bila kujali amezaliwa wapi, anastahili kupata chanjo na dawa za kuokoa maisha.”

Mkuu wa kitengo cha afya ya watoto wachanga na watoto katika wizara hiyo Caroline Mwangi anasema kuwa, nimonia ndiyo chanzo kuu la vifo kwa watoto baada ya kipindi cha kuzaliwa ila ugonjwa huu haujawekezwa katika mwonekano, kifedha, na ufadhili wa utafiti.

Hii imeilazimu wizara kuanzisha na kuongeza afua ambazo zina athari ya muda mrefu katika kupunguza visababishi hivi kulingana na mifumo ya afua za nimonia za kulinda, kuzuia na kutibu.

Mwakilishi wa Unicef ​​nchini Jeanne Lokenga alisema kwamba, hakuna kisingizio kwa nini baadhi ya watoto hawawezi kupata dawa za kuokoa maisha akisema kupunguza nimonia kunategemea mafanikio ya huduma za afya kwa wote.

Kiwango cha sasa cha vifo vya watoto wachanga nchini Kenya ni vifo 30 kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa wakiwa hai, sawa na asilimia 3.47 kutoka 2021.

Kiwango cha vifo vya watoto wachanga nchini Kenya mwaka 2021 kilikuwa vifo 32.9 kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa wakiwa hai, asilimia 3.36 kutoka 2020.

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *