mtoto.news

Wazazi na Walezi Wanapaswa Kuwalinda Watoto Wakati Wa Likizo Ndefu

November 25, 2022

Wazazi na walezi wahimizwa kuwalinda watoto wao

Wanafunzi wote washarudi majumbani mwao kwa likizo ndefu  ambayo inakusudiwa kumalizika mwisho wa January mwaka Ujao.

Hofu na wasiwasi unaongezeka juu ya utovu wa nidhamu wa watoto wakati huu wa likizo ndefu kwani mara nyingi shule huwafanya watoto kuwa na shughuli nyingi na huwaweka mbali na maovu, na hivyo kupunguza shinikizo kwa wazazi.

Na hivyo, wakati wa mapumziko haya marefu, tunawahimiza wazazi kuingilia kati na kutekeleza jukumu lao. Jamii si mlinzi wa watoto kwani siku hizi watoto wengi wanalelewa katika mazingira magumu sana.

Isitoshe, uhalifu umeongezeka, utekaji nyara wa watoto na mahitaji ya fidia yanaongezeka, dawa za kulevya zinapatikana kwa urahisi, maudhui machafu kwenye majukwaa mbalimbali ya vyombo vya habari yametapakaa, hii ikiwaacha watoto kwenye mazingira magumu.

Licha ya hayo, sasa hivi kuna athari mbalimbali za mabadiliko ya hali ya hewa, ikiwemo ajira kwa watoto, Mimba za mapema, Ndoa za mapema na kadhalika. Watoto wengi wanajitwika kwenye shimo la mapenzi wakihadawa na pesa kidogo, hasa wakati huu ambapo ni vigumu kumudu mahitaji ya kimsingi.

Wazazi lazima wawalinde mabinti zao kutokana na wapotoshaji na walala hoi, hususan wakati huu wa sherehe za kuvuka mwaka, wakati kuna starehe kadha wa kadha, na madawa ya kulevya yasiyoisha.

Ni vizuri kuwaacha watoto waweze kuwa na furaha na kusherehekea wakati wa likizo, lakini wazazi pia wanafaa kuwaangalia na kuwafuatilia watoto wao kwa ukaribu.

 

 

 

 

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *