mtoto.news

Mataifa 12 ya Afrika yaahidi kutokomeza VVU kwa watoto ifikapo mwaka 2030

February 27, 2023

picha: UNICEF

Mawaziri na wawakilishi kutoka nchi 12 za Afrika wamejitolea  na kuweka mipango ya kumaliza UKIMWI kwa watoto ifikapo mwaka 2030.


Nchi hizo ziliahidi kwamba, zitahakikisha watoto wote wenye VVU wanapata matibabu ya kuokoa maisha na hata akina mama wanaoishi na ugonjwa huo hawataweza kuwasambazia watoto wao. Katika taarifa ya pamoja baada ya mkutano ulioandaliwa na Tanzania, washirika wa kimataifa waliahidi kuwa, wataisaidia nchi katika kutekeleza mipango hiyo, ambayo ilitolewa katika mkutano wa kwanza wa mawaziri wa Umoja wa Kimataifa wa kukomesha UKIMWI kwa watoto.

“Muungano huo utafanya kazi katika kuleta maendeleo katika kipindi cha miaka saba ijayo, ili kuhakikisha kuwa lengo la 2030 linafikiwa,” taarifa hiyo ilisoma.

Nchi 12 zenye mzigo mkubwa wa VVU zilizojiunga na muungano huo katika awamu ya kwanza ni Angola, Cameroon, Côte d’Ivoire, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Kenya, Msumbiji, Nigeria, Afrika Kusini, Tanzania, Uganda, Zambia, na Zimbabwe. Waziri wa Afya Susan Nakhumicha alitumia kongamano hilo na kuthibitisha kujitolea kwa Kenya kuwa mstari wa mbele katika kukomesha maambukizi ya VVU na UKIMWI miongoni mwa watoto ifikapo mwaka wa 2030.

Waziri huyo  alisisitiza juhudi za serikali katika kutumia teknolojia za kidijitali katika kuhakikisha upatikanaji wa matibabu na matunzo kwa kina mama wajawazito na wanaonyonyesha, kutoa fursa ya upimaji na matibabu kwa watoto wote na vijana wanaoishi na VVU. Nakhumicha alionyesha zaidi, mbinu bora za kukomesha unyanyapaa, bajeti za kuzuia UKIMWI kwa watoto na kufuatilia maendeleo ya hali hiyo hiyo.

Hivi sasa, duniani kote, kila baada ya dakika tano kuna mtoto anafariki kutokana na sababu zinazohusiana na UKIMWI, huku asilimia nusu (52%) tu ya watoto wanaoishi na VVU wako kwenye matibabu ya kuokoa maisha.

Mwaka 2021, watoto walichangia asilimia 15 ya vifo vyote vinavyohusiana na UKIMWI licha ya ukweli wa kwamba, watoto ni asilimia nne tu ya idadi ya watu wanaoishi na VVU. Katika kipindi hicho hicho, watoto 160,000 walipata VVU.

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *