mtoto.news

Je elimu ya ngono ni muhimu kwa watoto?

March 7, 2023

 

Wazazi lazima wathamini jukumu lao la kipekee katika ujamaa wa watoto wao

Kulingana na Utafiti wa Demografia na Afya wa Kenya wa 2022, asilimia 15 ya wasichana wenye umri wa kati ya miaka 15 na 19 wamewahi kupata mimba. Takwimu hii huongezeka kila wanakuwa wakubwa kutoka asilimia 3 kati ya watoto wa miaka 15 hadi asilimia 31 kati ya wale wenye umri wa miaka 19.

Hii ni dalili tosha kwamba kama wazazi na walezi, kuna haja ya kuwa na mazungumzo yanayolingana na umri, kuhusu ngono. Tunaishi katika enzi ambazo watoto wanaonyeshwa habari hizi kupitia majukwaa tofauti, kama vile mtandaoni na vyombo vya habari, wenzi wao walio na miaka sawa na wao, na hata wazee na njia nyinginezo nyingi. Hii ina maana kwamba, tunakuza kizazi cha wadadisi na ndiposa ni muhimu kuwa na elimu ya ngono inayolingana na umri.

Hata hivyo, utamaduni ni miongoni mwa vikwazo vingi vinavyoathiri elimu ya ngono katika jamii yetu kwani maadili hayo huunda maarifa yetu, imani, na mazoea ya kujamiiana . Ushawishi wa awali zaidi juu ya ujinsia wetu ni kanuni za ngono za nyumbani na za kijamii ambazo tunakuzwa nazo na kisha baadae kuzipitisha kwa watoto . Hii inawawia vigumu wazazi katika kuwaelimisha watoto kuhusu ujinsia.

Walakini, wazazi lazima wathamini jukumu lao la kipekee katika ujamaa wa watoto wao. Hii ni pamoja na kuunda mtazamo wao wa ulimwengu kuhusu ngono. Tunahitaji kufahamu kwamba kama mzazi, watoto wako wanaweza kukuona kama mamlaka, au kama chanzo cha habari kinachoaminika, isitoshe, mzazi ni mahali salama kwao kupata habari kama hizo.

Changamoto kubwa tuliyonayo wakati wa safari hii ni hadithi ya kwamba, wakati tunazungumza na watoto kuhusu ngono basi huwa ni sawa na kuwapa ruhusa ya kujihusisha nayo. Ila hapana, wazazi wanafaa kutoa taarifa sahihi ili kuwalinda watoto kutokana na walawiti, udadisi na mengineo.  Tunahitaji kufahamu kwamba ikiwa hatutoi elimu ya ngono inayolingana na umri kwa watoto wetu basi watoto hao watakuwa mawindo ya mtandao, wenzi wao na ulimwengu wa nje ambao utatoa mafunzo ya ngono ambayo yanaweza yasifaulu vizuri.

Elimu ya ngono haihusu tu tendo la ngono bali pia inahusu mambo kama vile ukuaji wa mwili, uthabiti wa mwili, kujiamini, mahusiano, mawasiliano ya ujuzi wa kibinafsi, tabia ya ngono na jamii na utamaduni.  Tunaweza tu kuwalinda watoto wetu kwa kuwawezesha kuelewa ili kujua mguso usiofaa ni nini na ni upi. Kwa hivyo ni muhimu kwa watoto kuelewa miili yao na kujua ni wakati gani wanapaswa kumwambia mama, baba au mlezi wakati mtu anaingilia faragha yao. Hilo huweka msingi mzuri wa mazungumzo ya baadaye juu ya mambo ya ngono.- Dr Maureen Akolo

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *