mtoto.news

Watoto Wasishirikishwe Kwenye Maandamano

March 27, 2023

Photo from 2017 Post-Elections violence
Picha kutoka 2017 Vurugu za baada ya Uchaguzi

Wakati migogoro inapotokea, basi watoto ndio waumiao zaidi.


Jumatatu tarehe 20 2023 wiki iliyopita, kiongozi wa upinzani Raila Odinga, aliitisha Maandamano ya nchi nzima ili kupinga kupanda kwa gharama ya maisha nchini Kenya na ushindi wa rais William Ruto katika uchaguzi.

Ikifwatia habari inayosema kwamba mwanafunzi wa chuo kikuu aliuawa huku zaidi ya watu 200 kukamatwa katika maandamano hayo, hofu kuu inaangukia maandamano haya kwani mwisho wa siku maandamano haya huleta vurugu, majeraha na hata vifo.

Isitoshe, kiongozi mpinzani Bwana Odinga, alinena kwamba maandamano hayo yanatarajiwa kufanyika kila jumatatu kwa wiki kadhaa. Huu ni wakati nyeti mno kwa kila mwananchi, kwani watoto wengi  walishindwa kwenda shuleni huku wengine wao wakishiriki maandamano hayo pamoja na wazazi wao au walezi wao.

Wananchi wengi wameonyesha wasiwasi wao mitandaoni baada ya picha inayooshesha mzazi na mtoto wake kwenye maandamano ya leo kusambaa mitandaoni.

Aidha wazazi wengine wameonyesha hofu yao juu ya watoto wao wanaoenda shuleni leo hii, kwa kuwaonya polisi kupitia mtandao wa twitter kwamba, wasirushe vitoa machozi na mawe kwani hilo linaweza kuwadhuru watoto, huku wakisisitiza kwamba, kila mtoto ana haki ya ulinzi anapoenda shuleni.

Hata hivyo, viongozi wa kidini, miungano na kisiasa wanawataka Mheshimiwa Ruto na Raila kuketi chini na kuanzisha mazungumzo ili kunusuru nchi dhidi ya machafuko. Viongozi hao walisema kwamba, kizazi kijacho kitawawajibisha iwapo misimamo yao mikali itateketeza nchi.

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *