mtoto.news

Mashirika Ya Hifadhi Kutumia Sh78 Milioni Kwa Watoto Wanaoishi Katika Mazingira Magumu

May 9, 2023

Zaidi ya wanafunzi 12,000 wenye uhitaji kutoka kaunti za Marsabit, Isiolo, Samburu na Laikipia watanufaika na ufadhili kutoka kwa shirika la Northern Rangeland Trust (NRT) ili kufadhili elimu yao. Afisa mkuu mtendaji wa NRT Tom Lalampaa alisema kuwa, shirika hilo litatumia milioni Sh78.5 kwa wanafunzi 12,557 wanaohitaji.

Bw Lalampaa alisema kuwa, wahafidhina 18 wametanguliza elimu miongoni mwa jamii za wafugaji kwa nia ya kuwashauri wawe viongozi wa kutegemewa wa siku zijazo. Alisema kuwa shirika lake linatambua jukumu la wanawake miongoni mwa wafugaji na NRT inaweka elimu, afya na usalama katika ajenda zake, hatua ambayo imeleta mabadiliko chanya katika eneo hilo.

Bosi huyo wa NRT ambaye alikuwa akihutubia kongamano la wanawake huko Isiolo alisema kwamba shirika hilo limekuwa likiwawezesha wanawake hao kwa ujuzi wa kutengeza shanga kama njia ya kupunguza umaskini miongoni mwa jamii na pia kupunguza athari za ukame katika eneo hilo.

Aliongeza kuwa Wahifadhi wamekuwa wakishirikiana bega kwa bega na wananchi wa eneo hilo ili kuhakikisha kuwa wanyama walioibiwa wanapatikana na kurejeshwa kwa wamiliki kwa kuepusha migogoro miongoni mwa jamii.

Kuhusu ukame, Bi Elealo alisema kuwa faida kutokana na shughuli zao za kiuchumi iliwapa ujasiri lakini akawapa changamoto viongozi wa eneo hilo kuacha kuingiza siasa katika miradi ya NRT kwa kuwa shirika hilo limekuwa likinufaisha eneo hilo kijamii na kiuchumi.

                                                                                           Nakala-KNA

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *