mtoto.news

Takriban watoto 100,000 waathiriwa na mtetemeko wa ardhi nchini Morocco

September 12, 2023

Ripoti za awali zinaonyesha kwamba takriban watoto 100,000 wameathiriwa na tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba Moroko Ijumaa usiku wa kuamkia leo.

Hilo ni tukio kubwa zaidi la tetemeko kuwahi kukumba eneo hilo tangu mwaka wa 1960. Kama ilivyo kwa matetemeko yote makubwa ya ardhi, kuna uwezekano wa kutokea mitetemeko ya baadaye katika siku na wiki zijazo, jambo ambalo limewaweka watoto na familia katika hatari zaidi.

Kulingana na UNICEF, tetemeko hilo lenye nguvu ya 6.8 lilitokea masaa ya saa tano usiku tarehe 8 Septemba, wakati ambapo watoto na familia nyingi walikuwa wamelala majumbani mwao. Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa zaidi ya watu 300,000 wameathirika huko Marrakesh na katika Milima ya Juu ya Atlas.

Kwa mujibu wa mamlaka, zaidi ya watu 2,600 wameuawa, wakiwemo watoto , huku maelfu ya watu wamejeruhiwa. Nambari hizi zinaweza kuongezeka kadri juhudi za uokoaji zinaendelea. Ingawa UNICEF bado haijajua idadi kamili ya watoto waliouawa na kujeruhiwa, makadirio ya hivi karibuni kutoka mwaka 2022 yanaonyesha kuwa watoto wanawakilisha karibu theluthi moja ya idadi ya watu nchini Morocco.

Nyumba nyingi mno zimeharibiwa, hii imelazimisha maelfu ya familia kuhama, huku hali ya hewa ikizidi kuwa baridi wakati wa usiku. Shule, hospitali, na miundombinu mingine ya elimu na matibabu imeathiriwa au kuharibiwa na tetemeko hilo, jambo ambalo linaweka watoto katika hatari zaidi.

Katika hali yoyote ya dharura, watoto huwa miongoni mwa walio hatarini zaidi. Watoto na familia zilizoathiriwa zitahitaji makazi, maji salama ya kunywa, usaidizi wa afya na matibabu, na msaada wa chakula na lishe kwa muda mrefu. Huduma za ulinzi wa watoto ikiwa ni pamoja na usaidizi wa kisaikolojia na kijamii zitakuwa muhimu katika kuwasaidia watoto na wazazi katika kushughulikia hali zao za kuhuzunisha. Kurejesha watoto shuleni pia ni muhimu mno.

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *