mtoto.news

GAZA: Zaidi ya Watoto 4,600 Wauwawa huku Karibia 9000 Wajeruhiwa

November 17, 2023

Mnamo juzi tarehe 15 mwezi wa 11, mwaka wa 2023, Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Catherine Russell alifanya Ziara maeneo ya Gaza ili kukutana na watoto, familia zao na wafanyakazi wa UNICEF.

“Nilichoona na kusikia kilinihuzunisha sana. Wakaazi wa Gaza wamestahimili mashambulizi ya mara kwa mara, hii ikiwemo kuuwawa, kupoteana na familia zao, Kufukuzwa majumbani mwao na mengineyo mengi” alinena Russel.

Cha kusikitisha zaidi ni kwamba,  Watoto milioni moja hawana upande wa kugeukia kwani Kanda ya Gaza hamna mahali salama pa kuwasitiri watoto hao! Wahusika wa mzozo huu wanafanya ukiukwaji mkubwa dhidi ya haki za watoto; haya ni pamoja na mauaji, ulemavu, utekaji nyara, mashambulizi dhidi ya shule na hospitali, na kunyimwa huduma za kibinadamu

“Zaidi ya watoto 4,600 wameripotiwa kuuawa, na karibu 9,000 wameripotiwa kujeruhiwa.”Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF aliendelea kunena

Watoto wengi wamepotea na inaaminika kuwa wamefukiwa chini ya vifusi vya majengo na nyumba zilizoanguka, haya ni matokeo ya kusikitisha ya matumizi ya silaha za milipuko katika maeneo yenye watu wengi. Wakati huo huo, watoto wachanga wanaohitaji uangalizi maalum wamekufa katika hospitali moja ya Gaza huku nguvu na vifaa vya matibabu vikiisha, na ghasia zinaendelea huku athari zikimiminika kiholela.

“Katika hospitali ya Al Naser huko Khan Yunis, nilikutana na wagonjwa na familia zilizohamishwa kutafuta makazi na usalama. Msichana mwenye umri wa miaka 16 aliniambia akiwa katika kitanda chake cha hospitali kwamba, mtaa wake ulikuwa umelipuliwa kwa mabomu. Alinusurika ila madaktari wanasema hataweza kutembea tena.”

“Katika wodi ya watoto wachanga ya hospitali hiyo, watoto wadogo walikuwa waking’ang’ania maisha kwenye incubators, kwani madaktari walikuwa na wasiwasi jinsi wangeweza kufanya mashine zifanye kazi bila mafuta.” Alisema Russell

Watu wengi ikiwemo watoto wanaishi katika makaazi yenye msongamano wa watu, huku maji yakiwa kidogo mno, ukosefu wa chakula cha kutosha na hata vyoo bora, hali ambayo inaweza kusababisha milipuko ya wagonjwa.

Ufunguzi wa mara kwa mara wa vivuko vya mpaka wa Gaza kwa shehena za misaada ya kibinadamu haitoshi kukidhi mahitaji yanayoongezeka. Na msimu wa baridi ukiwa umekaribia, hitaji la mafuta linaweza kuwa kali zaidi.

Ulinzi wa watoto unafaa kupewa kipaumbele, kwani wakati wa vita watoto ndio huathirika zaidi, watoto wanafaa kulindwa na kusaidiwa kulingana na sheria za kimataifa ya kibinadamu. Wahusika wa Vita hivi wanafa kukomesha hali hii ya kutisha

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *