Shughuli ya kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi waliofanya mtihani wa KCPE mwaka wa 2023 na wasiojiweza imeng’oa nanga leo hii kupitia shirika la KCB jijiini Nairobi.
Wanafunzi zaidi ya elfu kumi na wawiili walituma maombi yao, idadi ambayo ni kubwa zaidi kushuhudiwa na KCB huku wanafunzi takribani elfu moja tu wakitarajiwa kunufaika.
Ufadhili huo ambao umetolewa na afisa mkuu wa KCB Paul Russo uliongozwa na waziri wa elimu Ezekiel Machogu.
Zoezi hili ni la kumi na saba tangu ufadhili huu kuanzishwa na shirika la KCB mwaka wa 2007 huku ufadhili huo ukitarajiwa kuwafaidi wanafunzi wasiojiweza katika jamii kwenye magatuzi arubaini na saba nchini Kenya.
Arnold Fedha.
Leave a Reply