mtoto.news

Syria:Mlipuko wa kipindupindu wahatarisha Afya na Elimu ya Watoto

September 21, 2022

Shirika la Save the Children, lasema kwamba, maelfu ya watoto huko mashariki na kaskazini mwa Syria wako hatarini kutokana na kuenea kwa kasi kwa ugonjwa wa kipindupindu unaosababishwa na uhaba wa maji unaohusishwa na mabadiliko ya hali ya hewa na migogoro na matumizi ya maji machafu kutoka Mto Euphrates.

Takriban watu 24 wamefariki kutokana na ugonjwa huo unaosambazwa na maji huku maelfu kadhaa ya visa vinavyoshukiwa vimeripotiwa kote nchini kufikia tarehe 19 Septemba .

Mlipuko huo unaambatana na kurejea shuleni kwa watoto wengi nchini Syria mwezi huu, na hivyo kuweka afya na elimu ya watoto hatarini.

Ni mlipuko wa kwanza mkubwa wa ugonjwa huo nchini Syria katika kipindi cha muongo mmoja na unaenea kwa kasi.

Kesi ya kwanza ilithibitishwa katika mji unaoshikiliwa na upinzani wa Jarablous kaskazini mwa Syria jana. Kabla ya hili, Kaskazini na Kaskazini Magharibi mwa Syria haikuwa imeripoti kisa chochote katika mlipuko huu, ikionyesha kwamba uwezekano wa kesi katika maeneo mengine bado uko juu.

Mlipuko wa sasa unaeleweka kusababishwa na jamii kunywa maji yaliyoambukizwa na chakula kinachomwagiliwa na Mto Euphrates, ambao unakabiliwa na viwango vya chini vya mtiririko wa kihistoria hasa kutokana na ukame mbaya zaidi nchini Syria katika miongo kadhaa.

Kwa kuongezea, maji taka kutoka kwa jamii zinazopatikana kando ya mto kwa kiasi kikubwa huishia kwenye Mto Euphrates, na hivyo kuongeza uwezekano wa magonjwa kuenea.

Takriban nusu ya watu nchini Syria hutegemea vyanzo vya maji visivyo salama kukidhi mahitaji yao ya kila siku.

Shirika la Save the Children linaonya kwamba kuenea kwa kipindupindu kunatarajiwa kuendelea katika siku na wiki zijazo kutokana na uhaba mkubwa wa maji, mamilioni ya watu kutegemea Mto Euphrates kwa maji yao ya kunywa , mifumo ya afya na maji yenye matatizo.

katika nchi ambayo haina uwezo wa kukabiliana na mlipuko ulioenea , na ukosefu wa upatikanaji wa vifaa vya usafi kutokana na matatizo ya kiuchumi.

Beat Rohr, Mkurugenzi wa Muda wa Save the Children nchini anasema:

“Tutakumbwa na mlipuko mkubwa iwapo hatutachukua hatua sasa, mlipuko ambao tayari unazidisha mahitaji ya ulinzi wa watoto kote Syria, na kuongeza mateso yao.”

Shirika la Save the Children linatoa wito kwa wafadhili kuhamasisha ufadhili wa ziada ili kukabiliana na mlipuko huo na kupunguza athari zake kwa watoto, huku wakijiandaa kwa ongezeko la mahitaji ya kibinadamu kote nchini. Mbali na hayo, mlipuko huo unaashiria haja ya kubadili mwelekeo kuelekea kupona mapema na kurejesha huduma za kimsingi, ikiwa ni pamoja na maji na usafi wa mazingira.

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *