mtoto.news

Lamu: Hofu baada ya mimba za mapema kushika kasi

October 18, 2022

Wasichana wadogo wanapitia dhulma mbali mbali maeneo ya Hindi ikiwemo kupachikwa ujauzito wa mapema, – watoto ambao mara nyingi huangukia matatizo kadha wa kadha wakati wa kujifungua.

Mimba za mapema sio jambo geni nchini Kenya, ila kwa sasa, wakaazi wa maeneo ya Hindi huko Lamu wameonya hofu na wasiwasi mkuu baada ya wanafunzi sita kutoka shule ya upili ya Hindi kupachikwa mimba kwa pamoja.

Kulingana na citizen, Wasichana wadogo wanapitia dhulma mbali mbali maeneo ya Hindi ikiwemo kupachikwa ujauzito wa mapema, – watoto ambao mara nyingi huangukia matatizo kadha wa kadha wakati wa kujifungua.

Pendo(sio jina lake kamili) ambaye ana miaka 17, akiwa kidato cha pili katika shule ya upili ya Hindi, amejifungua mtoto mapema, mtoto akiwa na miezi saba tu.

Pendo amesema kuwa, mara nyingi mimba hizi za mapema hutokana na shida ya kupata masilahi ya kimsingi ikiwemo ukosefu wa chakula, sabuni na mengineyo. Hata hivyo, pendo amesema kwamba, ako tayari kukubali msaada wowote ule ili aweze kurudi shule.

Aidha, Jamii ya hindi ina mahusiano ya juu ya maambukizi ya maradhi ya ngono, huku vilabu na mangwe vikichochea maambukizi ya magonjwa ya ngono, mimba na unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wadogo.

 

 

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *