Unyanyasaji wa kijinsia na kesi za mauaji ya wanawake zinaendelea kuongezeka nchini Afrika Kusini huku wanaume “wakatili” nchini humo wakiwalenga watoto na wanawake wazee.
“Katika siku za hivi majuzi tumeona visa vya ubakaji na mauaji ya vikongwe, mama na nyanya zetu ambao wanakusudiwa kuheshimiwa na kutendewa utu,” Rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa, asema.
Ameyazungumza hayo wakati wa mkutano wa pili wa rais kuhusu Unyanyasaji wa Kijinsia na Mauaji ya Wanawake. Kulingana na rais, data kutoka kwa Huduma ya Polisi ya Afrika Kusini inaonyesha kuwa makosa ya ngono na ubakaji yaliongezeka kwa asilimia 13 kati ya 2017-18, na 2021-2022.
Mauaji ya wanawake na watoto pia yanaongezeka, alisema.
“Kati ya robo ya kwanza ya 2021 na robo ya kwanza ya 2022 kulikuwa na ongezeko la asilimia 52 la mauaji ya wanawake, na ongezeko la asilimia 46 la watoto waliouawa,” Bw Ramaphosa alisema, huku akitoa wito kwa wanaume kukomesha uhalifu huo.
“Vitendo hivi vya kinyama ni mashtaka ya aibu kwa wanaume wa nchi hii.”
Hata hivyo aliangazia baadhi ya mafanikio kutoka kwa mkutano wa mwisho wa urais mwaka wa 2018, ikiwa ni pamoja na mahakama 83 kuboreshwa hadi mahakama za makosa ya ngono.
Leave a Reply