Naam, mara nyingi kila mtu huimba, “Elimu kwa wote”, “Elimu ya bure”, ila ukweli wa mambo ni kwamba, elimu iko na bei ya juu mno, jambo linalowafanya watoto wengi wakose kupata masomo.
Ahadi ya elimu ya msingi na sekondari kwa wote ni mojawapo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu . Hata hivyo mwaka wa 2020, takriban watoto milioni 64 hawakusoma shule ya msingi, wakiwemo wasichana milioni 34. Zaidi ya watoto milioni 195 duniani kote hawakuweza kumudu masomo yao katika shule ya sekondari.
Aidha, Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ina viwango vya juu zaidi vya kutengwa kwa elimu kati ya kanda sita za mikoa inayoendelea. Zaidi ya moja nukta mbili ya watoto wa umri wa shule ya msingi hawajaenda shuleni, huku karibia asilimia 60 ya vijana kati ya umri wa miaka 15 na 17 hawako shuleni. Kuna vikwazo vingi vya elimu kwa kaya zenye kipato cha chini.
Mojawapo ni karo za shule, ambazo kwa bahati mbaya zimesalia kuenea katika shule nyingi Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa, na kumesababisha matatizo ya kifedha kwa familia.
Data mpya ya Global Findex inagundua kuwa zaidi ya nusu ambayo ni sawa na asilimia 54 ya watu wazima maeneo ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara wana wasiwasi mkubwa kuhusu kulipa karo ya shule, huku asilimia 29 wanasema kwamba, ada za shule ni wasiwasi wao mkubwa wa kifedha, isitoshe hii ni juu ya gharama za matibabu, kulipia uzee na gharama za kila mwezi. Katika nchi kadhaa za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, zikiwemo Kenya na Nigeria, ada za shule ndizo zinazoripotiwa kuwa na wasiwasi wa kifedha.
Barani Afrika, asilimia 21 ya wanafunzi wanasoma shule za kibinafsi, jambo ambalo uchumi hauruhusu kwa watoto wote. Hata katika nchi kama Uganda, ambayo inatoa elimu ya msingi bila malipo, wazazi bado wana gharama za shule za sare, ada za mitihani, utunzaji wa shule, vitabu, au hata kuajiri mwalimu wa ziada.
Kwa kuzingatia umuhimu wa elimu na changamoto ambazo kaya za kipato cha chini zinakabiliana nazo, ni suluhisho gani la kifedha linaweza kusaidia? Data ya Global Findex inapendekeza fursa tatu:
Leave a Reply