Naam, kuongezeka kwa viwango vya utapiamlo huwawacha watoto katika hatari ya kuambukizwa magonjwa hatari kama vile surua.
Wakishirikiana na Wizara ya Afya na Huduma za Kibinadamu na washirika, Shirika la Afya Duniani (WHO) linasaidia kazi ya wahudumu wa afya ya jamii 2,163 wanaotembelea takriban kaya laki tatu kila mwezi nchini Somalia ili kuangalia watoto wagonjwa, haswa watoto walioko katika kaya ambazo wazazi hawatembelei vituo vya afya kutafuta huduma za afya kwa watoto wao wagonjwa kutokana na sababu kadha wakadha.
Wahudumu hawa wa afya ya jamii, waliotumwa na WHO katika maeneo yaliyoathirika zaidi, wanatafuta watoto wagonjwa wanaoshukiwa kuwa na surua, nimonia, kuhara au wanaoshukiwa kuwa na kipindupindu na malaria.
Vilevile, wahudumu hawa huwachunguza watoto kwa dalili za utapiamlo mkali.
Utafutaji huu wa mara kwa mara husaidia jamii kutafuta huduma za afya kwa wakati, jambo ambalo huokoa maisha.
Njaa Yachochea Kuenezwa kwa Surua
Ukame unaoendelea katika Pembe ya Afrika, ambayo ripoti ya WHO hivi majuzi iliainisha kama dharura ya kiafya ya daraja la tatu, hii ikimaanisha kuwa, Ukame huu ni janga kubwa, janga linalowaacha watoto wakiwa na unyonge, njaa na kushambuliwa na magonjwa.
Kati ya watu milioni 6.1 kote nchini hawana uhakika wa chakula, huku karibia milioni 1.7 wanaathirika na njaa kali.
Takriban watoto milioni 1.4 wenye umri wa chini ya miaka 5, na zaidi ya wanawake 250,000 wajawazito na wanaonyonyesha wanahitaji matibabu na matunzo kutokana na utapiamlo.
Kulingana na Relief Web kuanzia mwanzo wa mwaka hadi wiki ya 21 ya 2022 (29 Mei 2022), vituo vya afya na wahudumu wa afya ya jamii waliripoti kesi 9,562 zilizoshukiwa kuwa za surua, huku 7,650 (80%) kati yao wakiwa na umri wa chini ya miaka 5.
Idadi kubwa zaidi ya kesi zimeripotiwa kutoka Puntland, Jimbo la Kusini Magharibi na Banadir.
“Tunajizatiti zaidi kufikia kila mtoto ambaye maisha yake yanaweza kuokolewa na kulindwa kutokana na surua na chanjo zingine.
Katika kipindi cha miezi 4 ya operesheni yetu iliyoimarishwa ardhini, zaidi ya watoto 92,000 wamechanjwa dhidi ya chanjo za utotoni ikiwa ni pamoja na surua. Takriban watoto 19,000 kati ya hawa walitambuliwa kwamba hawajapokea chanjo yoyote katika maisha yao. Hii ikichachia kuenezwa kwa magonjwa kama vile surua. Kwa hiyo, tunamfikia kila mtoto katika wilaya hizi zilizoathiriwa na ukame na kumchanja dhidi ya surua na chanjo nyinginezo za utotoni.’
WHO
Faida za chanjo
Ukame unaoendelea nchini Somalia unaathiri maisha na afya ya mamilioni ya Wasomali.
Kama vibarua wa kawaida, Ilmo na mumewe hawapati pesa nyingi. Tangu ukame uanze, wameona vigumu zaidi kupata kazi za kujikimu kimaisha, na sasa wakiwa na watoto wawili wagonjwa, ambao walipata homa kali, kikohozi, maumivu ya koo, mafua na macho yenye majimaji hivi majuzi, dalili za ugonjwa wa surua, walilazimika kuishi kwa mlo mmoja kwa siku.
Watoto wa Ilmo walipata bahati ya kupata uangalizi, lakini kuna watoto ambao hawapati msaada kwa wakati, pamoja na familia nyingi ambazo zimeingia kwenye umaskini kutokana na kujaribu kushughulikia mahitaji yao ya afya.
Leave a Reply