mtoto.news

Tuwache kubagua watoto albino kwa sababu pia hao wanaweza kufaulu maishani.

August 18, 2022

Kulingana na ripoti ya Deutsche Welle, zeruzeru au kwa kingereza albino husababishwa na upungufu wa chembechembe za rangi ya ngozi, nywele na hata macho.

Hali hii ya zeruzeru hutokea ikiwa kuna historia ya hali hiyo katika familia. Albino aghalabu wana matatizo ya macho. Hii ni kuwa huwa hawaoni mbali au hawaoni karibu japo miwani huweza kusaidia tatizo hilo.

Ingawa albino huwa wanaangaliwa kama walemavu. Kuna baadhi ya watoto albino ambao wameweza kuonyesha kuwa licha ya ubaguzi wanaopitia katika shule na jamii, pia hao wanaweza kufaulu maishani.

Mfano ni Goldalyn Kakuya ambaye mwaka wa elfu mbili kumi na saba aliweza kuibuka msichana wa kwanza kuongoza mtihani wa kitaifa wa KCPE na maksi mia nne hamsini na tano. Mwaka wa elfu mbili kumi na tisa, Kakuya aliweza kupewa ufadhiwa na mke wa rais Margaret Kenyatta katika shule ya Brookhouse, ambapo aliweza kupata A katika somo nane nje ya somo kumi alizofanya.

Aidha, watoto albino wanafaa kuangaliwa na kuongozwa katika talanta zao Ili waweze kufaulu maishani kama watoto wengine.

 

 

 

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *